Wananchi wakishangaa msingi wa jengo la mama na mtoto linalodaiwa kujengwa chini ya kiwango uliojengwa kwa jumla ya shilingi milioni 36 |
Katika isiyo kuwa ya kawaida injinia wa halmashauri ya wilaya ya Geita Hamis Chande amenusurika kupigwa na wananchi wa kijiji cha Bugulula katika kata ya Bugulula wilayani Geita mkoani Geita baada ya kwenda kuangalia msingi wa jengo la mama na mtoto linalodaiwa kujengwa chini ya kiwango huku ikitumia kiasi kikubwa cha fedha ambazo ni asilimia 40 ya vijana wanaofanya kazi katika mgodi wa dhahabu GGM.
Tukio hilo limetokea jana wakati injinia huyo alipofika katika kijiji hicho akiwa na mafundi na vifaa kama cement na nondo kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa msingi huo ambao ni mbovu na huku akitaka kurekebisha sehemu chache.
Hata hivyo pamoja na jitihada zake hizo wananchi walikuwa wanataka msingi huo ubomolewe wote na uanze upya bila kujali pesa za kurudia watazipata wapi.
Baada ya kumuona injinia huyo anakuja kutoka mjini na kufika wananchi walipiga yowe wakitaka wananchi wakusanyike wapewe majibu ya kutosha kuhusu hatima ya msingi huo lakini injinia alikosa majibu baada ya wananchi kumzingira na kuanza kumsonga wakitaka kumpiga wakidai naye ni wale wale wanaokula pesa za wananchi kwa kujinufaisha wao hali ambayo ilizua tafrani kubwa kwa injinia huyo.
Wakizungumza kwa uchungu wananchi walisikika wakisema wao hawataki kurekebishwa kwa msingi bali wanataka msingi ubomolewe na urudiwe kujengwa upya kwani sh milioni 36 ni pesa nyingi ambazo wanadai zimejenga msingi na huku msingi ukiwa umebomoka na kutitia.
Mwananchi mmoja ambaye hakuta kutajwa jina lake alisema wizi huo ni mkubwa sana lakini akamtupia lawama diwani wa kata hiyo ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri kwa kitendo cha kupokea taarifa kutoka kwa mtendaji wake wa kata akidai msingi umekamilika asilimia mia moja kumbe ni uongo mtupu.
Mwandishi mimi kama mwananchi nashaangaa hawa viongozi wetu sijui wana matatizo gani tumefunga ofisi kwa sababu ya wizi watu wanatembea na mihuri mifukoni mwao msingi huu eti milioni 36 tusaidieni jamani lakini akashukuru gazeti la Tanzania Daima kwa kuibua ubadhilifu huu japo mwandishi wake amekuwa na wakati mgumu.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Geita Bw Ali Kidwaka alipoulizwa kwanini amemtuma injinia wake kwenda na mafundi wakati aliyetakiwa kwenda ni mkandarasi alisema kuwa yeye hakumtuma kwenda na mafundi wala kuongea kitu chochote bali alimtuma akakague tu na kurudisha majibu.
"Mimi nashaanga kusikia kaenda na mafundi",alisema Kidwaka.
Hata hivyo alisema yeye kama mkurugenzi msingi huo utabomolewa na kujengwa upya.
Katika vurugu hizo hakuna aliyejeruhiwa ambapo jeshi la polisi kutoka katika kituo kikuu cha wilaya ya Geita walifika wakiwa gari NO PT 1166 ambapo OSS wa kituo hicho Hikongo Joshua akiwa na askari wake 3 alimwamuru injinia kuondoka naye katika eneo hilo.
Na Valence Robert wa Malunde1 Blog- Geita