Wapenzi wengi wa filamu duniani watakuwa wanalitambua jina lake ambapo kwa Tanzania ni maarufu zaidi uswahilini lakini duniani ndio anatajwa kuwa muigizaji anayejulikana zaidi.
Jina lake ni Shahrukh Khan ambae ni mwigizaji wa filamu kutoka India ambapo jana ametengeneza headlines baada ya kutajwa na jarida la maswala ya fedha la Wealth-X la Singapore ndio mwigizaji tajiri zaidi Asia pia anashika nafasi ya pili duniani nyuma ya comedian Jerry Seinfeld ambaye ana utajiri wa dola za kimarekani milioni 820.
Khan ambaye ni maarufu kwa jina la Kingh Khan ana utajiri wa $600m akiwa kawazidi waigizaji wakubwa Hollywood kama Tom Cruise mwenye $480 million, akiwafuatia na Johny Depp na Tyler Perry ambao wote wana $450 million.
Social Plugin