HAYA NDIYO MAMBO 6 AMBAYO WANAUME HAWAPENDI KUFANYIWA NA WENZI WAO

Haya ni kwa mujibu wa mshauri wa masuala ya mahusiano, ndoa na vijana Frederick Kyara.

Hizi ni baadhi tu nakuwekea hapa japo kuna vitu pia wanawake hawavipendi kutoka kwa wenzi wao wanaume.

1. Wanaume hawapendi kuambiwa cha kufanya na wenzi wao
Mwanamke unapotaka mwanaume afanye jambo usimwambie alifanye bali fanya kama una mpa ushauri. Kwamba John hivi kwa nini tusiweke balbu hapa kwenye korido maana kuna giza kweli. Badala ya hivi wewe John huoni hapa kwenye korido kuna giza balbu imeungua mwezi sasa hujabadilisha kwa nini? Weka balbu bwana. Atafanya au asifanye kabisa kwa sababu umemwambia cha kufanya.

2. Wanaume hawapendi mwenzi mwenye makelele, mlalamishi
Yeye ni kulalamika kuanzia Jumatatu hadi Jumapili. Japo wanawake nao wanasema kuna wanaume walalamishii balaaa. Na wenye gubu wanasusa kula mpaka kuongea wanawanunia wake zao mmmmh!

3. Wanaume hawapendi mwenzi mchafu
Mchafu wa mwili wake na hata nyumbani kwenye suala la kutunza nyumba wanayoishi. Uchafu hufanya mwanamke apoteze mvuto.

4. Wanaume hawapendi mwenzi mbishi
Japo na wanawake wanasema wanaume ndio wabishi zaidi. Utampa mwanaume ushauri lakini haufanyii kazi ubishi mwingi.

5. Wanaume hawapendi kuamrishwa na mwenzi wao
Mwenzi mbabe anaetoa amri na kumtawala hawataki.

6. Wanaume hawapendi kuhisiwa hisiwa na kusachiwa sachiwa
Kumpekua kwenye simu, mifuko ya suruali kwamba unamulika mwizi. Hawapendi, tena pengine hawajafanya jambo la kuwafanya wahisiwe vibaya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم