Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Hii kali!! TAZAMA PICHA FISI KAJIFICHA KWENYE TUMBO LA TEMBO AKIOGOPA KUKAMATWA NA SIMBA



  

Hapa Fisi alikuwa anasikilizia kutoka Tumboni kwa Tembo huku akiangalia kama Simba yupo Nje



Hapa ilikuwa pata shika
 
Simba akiwa anamsikilizia Fisi atoke
Alipopata Nafasi tuu... Fisi huyo alichomokaa
  
 
Ana kwa ana na Simba
 

Simba huyooo anamkimbiza Fisi....  

Katika kujiokoa kwenye hatari yeyote ile si tu watu ambao wanaweza kupata wazo la ajabu la kutenda ilimradi tu kuepukana na mauti, fisi mmoja aliyekuwa katika lishe yake alijikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimika kujificha kwenye tumbo la mzogo wa tembo ili kumkwepa simba dume aliyemvamia ghafla.


Fisi huyo aliyaona mauti yaleeeeee, lakini aliona ni heri kukaa ndani ya tumbo la tembo kulikoni kuliwa na simba. picha zifuatazo zinaonyesha namna fisi huyo alivyojificha na baadae kufanikiwa kukimbia baada ya kupata upenyo. Tukio hilo halijatokea mbali bali ni kule Masai Mara, pata uhondo huo.


Na Stratton Hatfield. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com