Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HUYU HAPA NDIYO KAMISHINA MKUU WA MAMLAKA YA MAPATO ALIYETEULIWA NA RAIS KIKWETE

 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bwana Rished BADE.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni  Sefue, uteulzi huu unaanza tarehe 06 Mei, 2014.  Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu tarehe 14 Desemba, 2013.

Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.

Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato kama ifuatavyo:-

-Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.
-Juni,2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.
-Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.

-Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).

-Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)
-Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank Plc Emerging Markets.

-Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance
Company.

Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).

Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.

Imetolewa
na:
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu - Dar es Salaam.
08 Mei, 2014 - See more at: http://mwanaharakatimzalendo.blogspot.com/2014/05/rais-kikwete-amteua-rished-bade-kuwa.html#.U2t5LoGSz6I

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com