Klabu ya Manchester United imemtangaza kocha Louis Van Gaal kuwa ndiye Meneja na kocha mpya wa timu kwa msimu ujao,hatua hiyo inakuja wiki kadhaa baada ya klabu hiyo kumtimua David Moyes.
Sababu kubwa ya kutimuliwa kwa Moyes ni kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya ya timu hiyo kwa msimu uliopita,Louis Van Gaal ambaye ni kocha wa zaman wa timu za Ajax,Bayern na Fc Barcelona na kawa sasa anaifundisha timu ya taifa ya Uholanzi.
Anategemewa kujiunga na Manchester United mara baada ya kushiriki kwenye michuano ya kombe la dunia ingawa kwa sasa Louis Van Gaal amesaini mkataba wa miaka 3 na amemteua Ryan Giggs kuwa kocha msaidizi.
Social Plugin