Inatisha Geita!! MLINZI AUAWA KIKATILI KWA KUCHINJWA AKIWA KAZINI



Ikiwa  ni mwezi mmoja tangu mlinzi wa kampuni ya K.K.security mjini Geita kuchinjwa   hadi kufa na mwili wake kutupwa kwenye mgahawa chini ya meza katika eneo la Mbugani katika Kata ya Kalangalala   mkoani hapa, mlinzi mwingine  ameuawa kwa kuchinjwa usiku wa kuamkia leo mjini hapa.

 Tukio hilo limetokea usiku wa wa kuamkia leo katika mtaa wa Shilabela ambapo mlinzi huyo aliyejulikana kwa jina la Juma Sunguta(48) anayeishi mtaa wa Moringe  amechinjwa na kuuawa wakati akiwa katika eneo lake la kazi  analolinda lililoko shilabela .

Imeelezwa kuwa  mlinzi huyo ameuawa lakini  wauaji hao hawakuchukua kitu chochote zaidi ya kumchinja na kuondoka.

Baadhi ya watu wa eneo hilo waliioongea na mwandishi wa habari hizi baada ya kufika kwenye eneo la tukio wamedai kuwa huenda ni chuki za kulipizana visasi kwa sababu hapo kazini alikuwa anafanya kazi vizuri.

Afisa mtendaji wa kata ya Kalangalala Hussen Hamadi aliyefika kwenye eneo la tukio amesema kuwa yeye amepigiwa simu asubuhi kuwepo kwa tukio hili na alipoenda akakuta marehemu ametupwa nje ya maduka huku shingo ikiwa imechinjwa .

Aidha  Hamad ameongeza kuwa hali hiyo inasikitisha katika kata yake kwani hivi karibuni mlinzi mwingine naye aliuawa eneo la mbugani kwa hiyo kuna kila sababu ya kutafuta chanzo cha matukio hayo. 

Baadhi ya wakazi waliokuwa katika eneo  hilo ambapo ni eneo la maduka alipokuwa analinda marehemu  wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa  matukio ya mauaji yamekuwa mengi na hivyo kuishi kwa wasiwasi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa kamishina msaidizi Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini waliofanya unyama huo na kisha wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Na Valence Robert Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم