|
Ni katikati ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga -Ujenzi wa barabara ukiwa unaendelea ambapo leo mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick
bwana Brad Gordon (hayupo pichani) amekagua ujenzi wa barabara unaoendelea mjini Kahama,mgodi huo ndiyo ukiwa ni wafadhili wa mradi huo ambao wametoa shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya ujenzi wa kilomita takribani 6 za barabara mjini Kahama mkoani Shinyanga
ambao umeanza mwezi Desemba mwaka jana(2013) na unatajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu(2014) ukiwa unasimamiwa na wakandarasi kutoka nchini China
|
|
Wa pili ni kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Benson Mpesya akiwaonesha barabara maafisa kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya African Barrick (wa kwanza kulia ni meneja uzalishaji kutoka kampuni ya uchimbaji madini
ya dhahabu ya African Barrick Peter
Geleta,wa tatu kutoka kulia ni mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon,wa pili kutoka kushoto ni Meneja wa
mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga bwana Philbert
Rweyemamu,wa kwanza kutoka kushoto ni meneja wa radio Kahama Marco Mipawa ambaye alikuwa miongoni wa waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara hiyo ya siku moja iliyolenga kuangalia namna ujenzi wa barabara unavyoendelea mjini Kahama
|
|
Ni katika barabara iliyoko mkabala kabisa na kanisa katoliki jimbo la Kahama lakini pia karibu kabisa na nyumbani kwa mkuu wa wilaya ya Kahama ambako pia ujenzi wa barabara unaendelea ukiwa umefadhiliwa na African Barrick Gold Mine ambao wametoa jumla ya shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya ujenzi wa barabara takribani kilomita 6 huku serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu ikitoa shilingi milioni 700. |
|
Kushoto ni mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon akizungumza wakati wa ziara yake mjini Kahama kukagua ujenzi wa barabara ambapo pamoja na mambo mengine alisema wananchi wa Kahama wanaendelea kushirikiana vizuri na kampuni hiyo ya uchimbaji madini na kuongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa barabara hakuna uchakachuaji mkubwa unaofanywa na wananchi hali ambayo inawapa hamasa ya kuendelea kufadhili miradi mbalimbali katika mji wa Kahama na maeneo mengine nchini |
|
Hakika mji wa Kahama sasa unakuwa katika muonekano mpya na wa kuvutia,hapa ni katikati ya mji wa Kahama kama unavyoona ujenzi wa barabara unaendelea ambapo wananchi wanasema sasa wameanza kuonja matunda ya migodi inayowazunguka ukiwemo mgodi wa Buzwagi na Bulyang'hulu katika wilaya hiyo ya Kahama |
|
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya( mwenye suti) akizungumza wakati wa ziara hiyo abapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwataka wakandarasi wazawa kuiga mfano wa wakandarasi wa kigeni (kutoka China) wanaojenga barabara hizo na sasa ujenzi unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu baada ya kuanza mwezi Desemba mwaka 2013 hivyo kukamilisha ujenzi kwa wakati uliopangwa huku akiwataka wakazi wa Kahama kuendelea kushirikiana na wafadhili wa ujenzi huo.Mbele ni bi afisa uhusiano mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Bi Blandina Mughezi akipiga picha za kumbukumbu |
|
Kazi ya ujenzi wa barabara mjini Kahama inaendelea greda /kijiko kinachota zege |
|
Hii ni barabara inayopita katika eneo la kituo cha Polisi mjini Kahama,kama unavyoona inapendeza kweli kweli pamoja na kwamba ujezi bado unaendelea.Ambapo kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick imetoa pesa nyingi(bilioni 3.2) kwa ajili ya ujenzi huo huku mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akiahidi kuwekwa kwa taa katika barabara hizo kwa ajili ya kuimarisha usalama nyakati za usiku |
|
Mitaro nayo inajengwa katika kuweka uimara wa barabara hizo zinazojengwa na ABG katika wilaya ya Kahama inayotajwa kuchangamka kuliko wilaya zote za mkoa wa Shinyanga huku uchumi wake pia ukitajwa kupanda kutokana na uwepo wa migodi ya Buzwagi na Bulyang'hulu inayomilikiwa na African Barrick Gold Mine(ABG) |
|
Katika ziara yake mjini Kahama,Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick,alifika katika maeneo ya karibu na Dispensary ya Igalilimi,maeneo ambayo pia kunajengwa barabara na ABG huku wakandarasi kutoka China wakifanya kazi kwa kasi kubwa ili kuhakikisha kuwa mradi huo wa ujenzi wa barabara unakamilika ifikapo mwezi Juni mwaka 2014 |
|
Katikati ya mji wa Kahama ambako kumejengwa barabara za lami na ABG |
|
Ujenzi wa barabara unaendelea,ambao unakwenda sambamba na ujenzi wa mitaro mjini Kahama |
|
Ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya(pichani) baada ya ziara hiyo ya siku moja ambapo aliushukuru uongozi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu African Barrick kwa kuwajengea barabara.Alisema ABGh hapa nchini inaongoza pia kwa kutoa ajira baada ya serikali lakini pia ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa umeme hapa nchini.Mpesya alitumia fursa hiyo kuwaomba ABG kuendelea kufadhili miradi bila kuchoka |
|
Mbele kushoto ni Meneja
uzalishaji kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick Peter Geleta,wa kwanza mbele kulia ni mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara hiyo ya siku moja (leo) kukagua ujenzi wa barabara mjini Kahama mkoani Shinyanga |
|
Picha ya pamoja baada ya kikao cha majumuisho ya ziara hiyo ya siku moja.Ziara hiyo ikiongozwa na mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon(wa pili kutoka kulia),pia walikuwepo maafisa mbalimbali kutoka mgodi wa dhahabu wa Buzwagi,mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya( wa tatu kutoka kulia(,meneja wa mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu(wa tatu kutoka kushoto) Meneja
uzalishaji ABG Peter
Geleta pamoja waandishi wa habari |
|
Picha ya pamoja-Kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika sekta mbalimbali hapa nchini kama vile sekta ya elimu,sekta ya michezo,sekta ya afya n.k hali ambayo inapelekea uhusiano kati ya kampuni hiyo(migodi) na wananchi wanaozunguka migodi.
Picha zote na Kadama Malunde wa malunde1 blog |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com