Kahama sasa kama Ulaya!! BARABARA ZAJENGWA KWA KASI YA AJABU NA KAMPUNI YA AFRICAN BARRICK GOLD MINE,MENEJA WA ABG AFANYA ZIARA KUKAGUA BARABARA HIZO,TUKIO ZIMA LIKO HAPA

Ni katikati ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga -Ujenzi wa barabara ukiwa unaendelea ambapo leo mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon (hayupo pichani) amekagua ujenzi wa barabara unaoendelea mjini Kahama,mgodi huo ndiyo ukiwa ni wafadhili wa mradi huo ambao wametoa shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya ujenzi wa kilomita takribani 6 za barabara mjini Kahama mkoani Shinyanga
ambao umeanza mwezi Desemba mwaka jana(2013) na unatajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu(2014) ukiwa unasimamiwa na wakandarasi kutoka nchini China
Wa pili ni kutoka kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Benson Mpesya akiwaonesha barabara maafisa kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya African Barrick (wa kwanza kulia ni meneja uzalishaji kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick  Peter Geleta,wa tatu kutoka kulia ni  mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon,wa pili kutoka kushoto ni  Meneja wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga bwana Philbert Rweyemamu,wa kwanza kutoka kushoto ni meneja wa radio Kahama Marco Mipawa ambaye alikuwa miongoni wa waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara hiyo ya siku moja iliyolenga kuangalia namna ujenzi wa barabara unavyoendelea mjini Kahama

Ni katika barabara iliyoko mkabala kabisa na kanisa katoliki jimbo la Kahama lakini pia karibu kabisa na nyumbani kwa mkuu wa wilaya ya Kahama ambako pia ujenzi wa barabara unaendelea ukiwa umefadhiliwa na African Barrick Gold Mine ambao wametoa jumla ya shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya ujenzi wa barabara takribani kilomita 6 huku serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu ikitoa shilingi milioni 700.
Kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon akizungumza wakati wa ziara yake mjini Kahama kukagua ujenzi wa barabara ambapo pamoja na mambo mengine alisema wananchi wa Kahama wanaendelea kushirikiana vizuri na kampuni hiyo ya uchimbaji madini na kuongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa barabara hakuna uchakachuaji mkubwa unaofanywa na wananchi hali ambayo inawapa hamasa ya kuendelea kufadhili miradi mbalimbali katika mji wa Kahama na maeneo mengine nchini


Hakika mji wa Kahama sasa unakuwa katika muonekano mpya na wa kuvutia,hapa ni katikati ya mji wa Kahama kama unavyoona ujenzi wa barabara unaendelea ambapo wananchi wanasema sasa wameanza kuonja matunda ya migodi inayowazunguka ukiwemo mgodi wa Buzwagi na Bulyang'hulu katika wilaya hiyo ya Kahama



Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya( mwenye suti) akizungumza wakati wa ziara hiyo abapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwataka wakandarasi wazawa kuiga mfano wa wakandarasi wa kigeni (kutoka China) wanaojenga barabara hizo na sasa ujenzi unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu baada ya kuanza mwezi Desemba mwaka 2013 hivyo kukamilisha ujenzi kwa wakati uliopangwa huku akiwataka wakazi wa Kahama kuendelea kushirikiana na wafadhili wa ujenzi huo.Mbele ni bi afisa uhusiano  mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Bi Blandina Mughezi akipiga picha za kumbukumbu 


Kazi ya ujenzi wa barabara mjini Kahama inaendelea greda /kijiko kinachota zege 
Hii ni barabara inayopita katika eneo la kituo cha Polisi mjini Kahama,kama unavyoona inapendeza kweli kweli pamoja na kwamba ujezi bado unaendelea.Ambapo kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick imetoa pesa nyingi(bilioni 3.2) kwa ajili ya ujenzi huo huku mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akiahidi kuwekwa kwa  taa katika barabara hizo kwa ajili ya kuimarisha usalama nyakati za usiku
Mitaro nayo inajengwa katika kuweka uimara wa barabara hizo zinazojengwa na ABG katika wilaya ya Kahama inayotajwa kuchangamka kuliko wilaya zote za mkoa wa Shinyanga huku uchumi wake pia ukitajwa kupanda kutokana na uwepo wa migodi ya Buzwagi na Bulyang'hulu inayomilikiwa na African Barrick Gold Mine(ABG)


Katika ziara yake mjini Kahama,Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick,alifika katika maeneo ya karibu na Dispensary ya Igalilimi,maeneo ambayo pia kunajengwa barabara na ABG huku wakandarasi kutoka China wakifanya kazi kwa kasi kubwa ili kuhakikisha kuwa mradi huo wa ujenzi wa barabara unakamilika ifikapo mwezi Juni mwaka 2014
Katikati ya mji wa Kahama ambako kumejengwa barabara za lami na ABG


Ujenzi wa barabara unaendelea,ambao unakwenda sambamba na ujenzi wa mitaro mjini Kahama
Ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya(pichani) baada ya ziara hiyo ya siku moja ambapo aliushukuru uongozi wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu African Barrick kwa kuwajengea barabara.Alisema ABGh hapa nchini inaongoza pia kwa kutoa ajira baada ya serikali lakini pia ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa umeme hapa nchini.Mpesya alitumia fursa hiyo kuwaomba ABG kuendelea kufadhili miradi bila kuchoka


Mbele kushoto ni Meneja uzalishaji kutoka kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick  Peter Geleta,wa kwanza mbele kulia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon wakati wa kikao cha majumuisho  ya ziara hiyo ya siku moja (leo) kukagua ujenzi wa barabara mjini Kahama mkoani Shinyanga


Picha ya pamoja baada ya kikao cha majumuisho ya ziara hiyo ya siku moja.Ziara hiyo ikiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick bwana Brad Gordon(wa pili kutoka kulia),pia walikuwepo maafisa mbalimbali kutoka mgodi wa dhahabu wa Buzwagi,mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya( wa tatu kutoka kulia(,meneja wa mgodi wa Buzwagi Philbert Rweyemamu(wa tatu kutoka kushoto) Meneja uzalishaji ABG Peter Geleta pamoja waandishi wa habari  
Picha ya pamoja-Kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika sekta mbalimbali hapa nchini kama vile sekta ya elimu,sekta ya michezo,sekta ya afya n.k hali ambayo inapelekea uhusiano kati ya kampuni hiyo(migodi) na wananchi wanaozunguka migodi.

Picha zote na Kadama Malunde wa malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم