KAMERA ZETU ZIMENASA HIKI MJINI KAHAMA MKOANI SHINYANGA,TAZAMA PICHA
Sunday, May 11, 2014
Mwandishi wa habari wa Malunde1 blog akiwa mjini Kahama mkoani Shinyanga alifanikiwa kunasa wanyama Punda wakiwa wamebebeshwa mzigo wa mapumba kwenye mkokoteni maarufu kwa jina la "MATELA" katika barabara za lami ,kama unavyoona pichani punda wa kwanza ameumia kwenye shingo yake lakini mwenye punda wala hajali na badala yake anambebesha mzigo na kumpitisha kwenye barabara za lami,huo ni ukatili dhidi ya wanyama.Ukatili wa dhidi ya wanyama mbali na kufanyika mjini Kahama pia unafanyika katika maeneo mengine mkoani Shinyanga. Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa malunde1 blog umebaini kuwa mjini Kahama kuna mikokoteni mingi inayovutwa na wanyama aina ya punda tena kwenye barabara za lami zinazoendelea kujengwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya African Barrick ambayo imetoa jumla ya shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami mjini Kahama. Je wahusika wa haki za wanyama mko wapi? je hamuoni kinachoendelea mjini Kahama?
PICHA ZOTE NA KADAMA MALUNDE WA MALUNDE1 BLOG
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin