NB PICHA HAIHUSIANI NA STORI |
Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Geita,Mkoani
Geita Busee Bwire ameingia katika kashfa nzito baada ya kuangusha gari la
polisi baada ya kuacha njia na kupinduka wakati akiliendesha likiwa na watuhumiwa
8 hali iliyopelekea watuhumiwa 6 kutoroka
muda mfupi baada ya ajali hiyo.
Ajali hiyo imetokea Julai 7
majira ya saa 2 usiku katika kijiji cha Bufunda,Tarafa ya Busanda Wilaya na
Mkoa wa Geita ambapo vyanzo vyetu vya habari kutoka eneo la tukio hilo vimedai
kuwa,chanzo cha ajali hiyo ambayo imefanywa siri kubwa ni mwendo kasi wa dereva
OCD Bwire.
Ajali hiyo imehusisha gari la polisi lenye
namba za usajili PT 1998, ambapo askari polisi watatu waliokuwa
ndani ya gari hiyo wamenusurika kufa huku mmoja kati yao aking'oka meno mawili
ya mbele baada ya kuacha njia na kupinduka wakati wakitokea kituo kidogo
cha polisi Nyarugusu kufuata watuhumiwa.
Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa,gari
hilo huendeshwa na PC Paulo,wa kituo cha Polisi Geita na ndiye aliyeliendesha
wakati likitokea Geita lakini wakati wakiwa kituo cha polisi Nyarugusu OCD
Bwire alilichukua gari hilo na kuliendesha yeye hadi wakati linapata ajali
wakielekea Geita mjini.
Imeelezwa kuwa,gari hilo lililokuwa
limepakia watuhumiwa wa makosa mbalimbali lilikuwa linawatoa kituo cha polisi
Nyarugusu na kuwahamishia kituo kikuu cha polisi Geita liliacha njia na
kupinduka baada ya Dereva ambaye ni OCD Bwire kumshinda kutokana na yeye kuwa
mgeni wa barabara hiyo.
Hata hivyo,mbali na OCD Bwire,askari
wengine wawili kutokujeruhiwa,katika ajali hiyo, askari mmoja aliyejulikana kwa
jina la Pc Linus wa kituo cha Nyarugusu alijeruhiwa baada ya meno yake mawili
ya mbele kung'oka.
Hata hivyo hali ya askari huyo aliyelazwa
katika hospitali ya Wilaya ya Geita kwa matibabu inaendelea vizuri.
Kaimu Mganga wa Hospitali ya Wilaya ya
Geita Dk Adam Sijaona alithibitisha kuwepo kwa majeruhi huyo hospitalini hapo
wodi ya Grade na kuahidi kutoa maendeleo halisi ya mgonjwa huyo mara
atakapomuona.
Gari hiyo,kwa sasa inafanyiwa matengenezo
kwa siri,tena usiku na mchana kwenye gereji moja bubu ya mjini Geita baada ya
kuvunjika kioo cha mbele na kubonyea upande wa kushoto ambako inapigwa rangi
upya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Joseph
Konyo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kudai kuwa watuhumiwa waliotoroka
ni watatu waliokuwa na makosa ya kuingia kwa jinai na kwamba jarada la
uchunguzi limefunguliwa na polisi inaendelea kuwasaka.
Hata hivyo,chanzo chetu cha habari
kimeeleza kuwa,taarifa iliyopelekwa kwa Kamanda imechakachuliwa kwani
watuhumiwa waliotoroka ni sita na kwamba jarada namba
GE/IR/2111/2014 limefunguliwa kituoni hapo kwa ajili ya kuwatafuta.
Imeelezwa,watuhumiwa wanane kati yao
sita waliotoroka baada ya ajali hiyo ambao ni pamoja na William
Michael,Charles Julius,Mussa Mashili,Joseph John,Nelson Raphael na Omari Sued.
Katika hatua nyingine imeelezwa mara
kadhaa Mkuu huyo wa polisi Wilaya ya Geita Bwire, amekuwa akizuiwa na uongozi
wa mkoa kuendesha gari hilo wanapokuwa kwenye oporesheni mbalimbali kwa sababu
za kiusalama.
Hata hivyo OCD Bwire,anadaiwa kukaidi
maelekezo hayo ya wakubwa zake mbali na kutambua kuwa akiwa kama kiongozi wa
juu wa jeshi hilo anapaswa kuendeshwa na si vinginevyo.
“Alishaonywa sana lakini hasikii...kama
unayonamba ya simu ya Kamanda aliyeondoka mpigie atakuambia..yaani alishamuonya
sana lakini hasikii na ndiyo maana askari wamekuwa wakikwepa kupanda gari hilo
iwapo anaendesha yeye maana mwendo wake huwa mkali sana'',Kilisema chanzo chetu
cha habari kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Na Valence Robert wa Malunde1 Blog Geita
Social Plugin