KIJANA AUAWA KIKATILI KWA KUKATWA KATWA MAPANGA BAADA YA KUNASWA AKISAFIRISHA NYAMA INAYODAIWA KUWA NI YA WIZI

 

Wananchi wenye hasira kali wamemuua mtu mmoja  aliyefahamika kwa jina moja la Daniel ambaye alikuwa ni  mkazi wa  manispaa ya mjini sumbawanga katika  mkoa wa  Rukwa kwa kile kinachodaiwa kusafirisha nyama ya ng'ombe iliyokuwa imeibwa na watu  wengine na ndipo marehemu aliponaswa na  kukatwakatwa na shoka na mapanga ..

Kamanda wa polisi  mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda akitoa  taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa kuwa  tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana saa tisa usiku katika kitongoji cha Malangali kilichopo mjini hapa.

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kata ya Malangali, Baziri Stima, alisema kuwa chanzo cha kijana huyo kuuawa ni kutokana na kunaswa akisafirisha nyama ya ng'ombe kwa kutumia usafiri wa pikipiki yake ambayo ilibeba nyama hiyo ambayo ilichinjiwa katika mistu wa malangali hivyo kuhisiwa kuwa ng'ombe aliyechinjwa alikuwa wa wizi.

 Inadaiwa kuwa baada ya kijana huyo kubeba mzigo wa kwanza, alirudia mzigo wa pili ndipo aliponaswa na kundi la watu na kuanza  kuhojiwa alikoitoa nyama hiyo ambapo wakati akijaribu kutoa maelezo ghafla watu hao walianza kumshushia kipigo huku wakitumia silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na shoka hadi alipofariki dunia kisha kuichoma moto pikipiki yake.

Inaelezwa kuwa kuuawa kwa kijana huyo kufuatia kuwepo kwa matukio ya mara kwa mara ya wizi wa mifugo hususani ng'ombe ambapo wakazi wa kitongoji hicho wamekuwa wakilalamika kuibiwa mifugo yao na baadhi ya watu kisha ng'ombe hao kuchinjwa katika eneo la msitu wa malangali nyakati za usiku wa manane.

Kwa upande wa kamanda wa polisi mkoa huo, alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuwabaina watu waliohusika na mauaji hayo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Mwaruanda alitoa rai kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi pindi wanapowakatama watu wanaowatuhumu kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu badala wawafikishe kituo cha polisi ili sheria ichukue mkondo wake.

Hili ni tukio la pili la kijana wa bodaboda kuuawa baada ya kubeba nyama inayodaiwa ilitokana na wizi wa ng'ombe, tukio la kwanza lilitokea katika kata ya Senga ambapo kijana mmoja auawa na kuchomwa moto na watu wasiojulikana kutokana na kunasawa akisafirisha nyama hiyo.

Na Elizabeth Ntambala, Sumbawanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post