Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIKONGWE WA MIAKA 70 AUAWA KIKATILI KWA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO HUKO MBEYA


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE”TAREHE 07.05.2014.
MZEE WA MIAKA 70 AUAWA KWA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO AKIWA NYUMBANI KWAKE
WATU WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA NCHINI ZAMBIA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA GOBOLE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MZEE WA MIAKA 70 ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FOLO MWALUSEPO MKAZI WA KIJIJI CHA IGUNDU WILAYA YA CHUNYA ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUMWAGIWA MAJI YA MOTO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA AKIWA NYUMBANI KWAKE.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.05.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA ISOKO, KIJIJI CHA IGUNDU, KATA NA TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA TUKIO HILI KINACHUNGUZWA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

KATIKA TUKIO LA PILI:

WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LUTIA KISAMBUKA @ MWAKAPETA (40) 2. VERONICA MTWEVE (41) NA 3. NIKUSEKELA MBOLYE (70) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISANGE WAMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T.599 ALH AINA YA MITSUBISHI CANTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NDINANI MWANGOLELA KUSHINDWA KUPANDA SEHEMU YENYE MWINUKO KUTOKANA NA UTELEZI NA KISHA KURUDI NYUMA NA KUPINDUKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 06.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISANGE, KATA YA ISANGE, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA ISANGE/MBIGILI. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WAWILI WALIPATA MAJERAHA, WALITIBIWA NA KURUHUSIWA. GARI HILO LILIKUWA LIMEBEBA MZIGO WA MADUMU 100 YA MAZIWA YENYE UJAZO WA LITA 20 PAMOJA NA MAGUNIA 10 YA MAHINDI NA VIAZI. DEREVA ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA MISAKO:

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA WAMEKAMATA SILAHA/ BUNDUKI MOJA AINA YA GOBOLE IKIWA NA RISASI TATU [03] ZA S/GUN.

KATIKA MSAKO HUO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:45 ASUBUHI HUKO ENEO LA CUSTOM-TUNDUMA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, MTUHUMIWA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA RIG MKAZI WA NAKONDE-ZAMBIA ALIKIMBIA MARA BAADA YA KUWAONA ASKARI HAO NA KUTUPA MFUKO ULIOKUWA NA SILAHA HIYO. 

AIDHA MTUHUMIWA MMOJA AITWAYE BARBARA CHUULU MWANS (45) MWALIMU SHULE YA SEKONDARI SINAZONGWE SOUTHERN PROVINCE ZAMBIA AMBAYE ALIKUWA NA MTUHUMIWA ALIYEKIMBIA AMEKAMATWA KWA MAHOJIANO ZAIDI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.

KATIKA MSAKO WA PILI ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 06.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA MTAA WA IGOGWE TUKUYU MJINI, KATA YA KAWETELE, TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. EMANUEL GIBSON (31) MKAZI WA IGOGWE NA 2. EMANUEL HELELA (27) MWALIMU SHULE YA SEKONDARI LUANGWA, MKAZI WA LUANGWA WAKIWA NA BHANGI MISOKOTO KUMI [10] SAWA NA UZITO WA GRAMU 50.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KAWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com