Kimenuka!!! BAVICHA GEITA WATOA TAMKO ZITO KUHUSU WALIOTAKA VIONGOZI WA UKAWA KUJITOA,WADAI HUO NI UHUNI TU


Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Geita Neema Stivin Chozaile wakati akitoa tamko mkoani Geita

Baraza la vijana la Chama cha Chadema mkoani Geita limetoa tamko juu ya upotoshaji wa mtu mmoja anayejiita Fikiri Migiyo juu ya kuwataka viongozi wa ngazi ya kitaifa kujitoa kwenye umoja wa katiba ya wananchi UKAWA na kusema kuwa huo ni uhuni wa mtu mmoja ambaye hawamjui hata kwenye chama chao.



Akizungumza na waandishi wa habari jana mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Geita Neema Stivin Chozaile amekanusha vikali habari hizo na kuziita ni uzushi mkubwa sana kwani wao kama bavicha hawajafanya mkutano na kutoa tamko kama hilo na kusema bavicha mkoa wa Geita haina katibu bali ina mwenyekiti tu sasahawajui huyo ametokea wapi.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa hata yeye alishangaa kuona habari hizo kwenye vyombo vya habari na kuongeza kuwa kitendo hicho cha mtu kujitambulisha na kujiita katibu wa Bavicha mkoa wa Geita ni kiovu na na kukiita cha kihuni na kumtaka kama anajijua ajisalimishe ndani ya siku saba kwani kutakuwa na uchunguzi mkubwa juu ya aliyevumisha uvumi huo.


Neema ameendelea kusema kuwa huenda ni Mbinu za CCM na waache mara moja kukichafua chama hicho na wao kama Bavicha mkoa wa Geita wanaiunga mkono asilimila miamoja muungano  wa vyama hivyo  na kuwata wananchi wa mkoa wa Geita kuacha kusikiliza poropaganda za watu wasiokuwa na msimamo kama CCM.
.
Kwa upande wa katibu wa chadema wilaya ya Geita Rogers Luhega amesema kuwa hizo ni mbinu chafu tu za watu wanaoweweseka na UKAWA ulivyojipanga kwa kuwakomboa wananchi kwani uchaguzi wa task force uliofanyika hivikaribuni mjini hapa hakuna jina la kiongozi huyo iwe wilayani ama mkoani na hatumjui kabisa sisi tunaendelea na vikao na wenzetu cuf kwa ajili ya mapokezi ya wageni wetu jumatatu ijayo.


Naye Abdalah Tungaraza mwanachama wa CUF ambaye pia ni Ukawa amelaani tamko la mtu huyo ambaye hajulikani hata anwani yake wala makazi yake na kuongeza kuwa sisi ukawa tutahakikisha hakuna mtu wakutuchonganisha kwa lolote lile. 

Uvumi huo umekuja na kuonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari  kukiwa ni siku chache viongozi wa ukawa kuanza ziara mkoani hapa kwa kutaka kuwaeleza watanzania juu ya kinachoendelea juu ya mchakato wa katiba .

NaValence Robert wa Malunde1 Blog -Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم