KUHUSU TAARIFA ZA KIFO CHA SHUJAA WA KAMERA MLIMANI TV , MAXMILLIAN NGOBE
Friday, May 23, 2014
Wingu zito latanda baada ya tasnia ya habari kupokea kwa uchungu na masikitiko makubwa, kifo cha mzee wetu Maxmilian John Ngobe aliyejulikana zaidi kama papaa Max ambaye amefariki leo asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata ni kwamba papaa Max amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Alikuwa ni mfanyakazi hodari kutoka Mlimani TV, hakika wanamlimani na wapenzi wa tasnia ya habari kwa ujumla wamemkosha shujaa, kipenzi cha wengi na msema kweli.
Alikuwa ni mpiga picha hodari wa Mlimani TV kwa muda mrefu sana, Tutakukumbuka daima kwa ucheshi wako na umakini wako katika kazi,hakika hukupenda utani kwenye kamera.
Alipenda kujulikana kama papaa Max na msiba utakuwa nyumbani kwa marehemu maeneo ya Tegeta jijini Dar es salaam
Mtandao huu wa Malunde1 Blog unawapa pole wote walioguswa kwa namna moja ama nyingine na msiba huu, familia, wafanyakazi wote wa Mlimani, wanafunzi wa shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
Mungu ailaze Roho ya marehemu Maximillian Ngube mahala pema peponi. Amina
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin