Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUMBE ANAYETUHUMIWA KUMBAKA SHEMEJI YAKE NI MUME WA FLORA MBASHA,SOMA HAPA

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha anayetuhumiwa kwa ubakaji.

JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17  ambaye ni yatima. 
Taarifa za tukio hilo ziliripotiwa Jumatatu saa 12 jioni katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule)  na  kufunguliwa kesi  yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/319/2014 na ya Jalada  la  Uchunguzi Na.TBT/IR/1865/2014, zikimtuhumu mwanamume huyo kwamba alimbaka binti huyo mara tatu na kumsababishia maumivu makali.
 
Binti huyo alifika katika kituo hicho cha polisi akiwa na ndugu zake wawili ambao walilalamika kwamba kulikuwa na jitihada kubwa kutoka upande wa mtuhumiwa wa kuzima kesi hiyo.
 
Akizungumza na mwanahabari  wetu  nje ya kituo hicho, binti huyo alisema shemejiye alimbaka mara ya kwanza, Ijumaa iliyopita na Jumapili alimbaka mara mbili ndani ya gari.
 
Alisema mara ya kwanza alikaa kimya baada ya mtuhumiwa kumtishia kwamba angemdhuru kama angetoa taarifa ya tukio hilo alilofanyiwa wakiwa sebuleni nyumbani kwake Tabata Kimanga, lakini aliamua kutoa taarifa kwa ndugu zake baada ya kubakwa mara ya pili.

Kauli  ya  Florah  Mbasha
Alipoulizwa  juzi Jumanne, mwimbaji huyo alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia kwa undani tuhuma zinazomkabili mumewe na kwamba alikuwa anajisikia vibaya kutokana na tukio hilo kuhusisha watu wake wa karibu.
 
“Of course (bila shaka), hili sio tukio zuri. Kwa sasa sina uwezo wa kuzungumza kwa sababu hili suala lipo Polisi. I am confused (nimechanganyikiwa), ukizingatia kwamba linasemekana kutokea wakati sikuwepo nyumbani, naomba tuzungumze baada ya akili kutulia,” alisema.
Vipimo vya hospitali
Siku  hiyo  ya  Jumatatu, baada ya tukio hilo kuripotiwa, mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Amana ambako alifunguliwa faili la matibabu na kupewa namba ya usajili 667. Aliingia chumba cha matibabu namba 21 kumuona daktari kwa ajili ya vipimo zaidi.
Matokeo ya vipimo yalionyesha kuwa binti huyo alikuwa amefanya ngono kwa nguvu. Katika fomu hiyo ya uchunguzi, daktari aliandika ‘High v5gina swab’.
 
Baada ya vipimo, familia ilirudi katika Kituo cha Polisi kupeleka matokeo ya vipimo vya daktari, hivyo kufungua faili la kesi lililopewa namba RB TBT/RB/319/2014 na namba TBT/IR/1865/2014. 

Juzi  Jumanne   binti huyo alikwenda tena Amana ambako alifanyiwa vipimo vilivyobaki vya VVU na mimba. Vipimo vya awali vya VVU vilionyesha kuwa hakuwa ameathirika na hakupata ujauzito.

Historia  ya  Mlalamikaji( binti )
Mlalamikaji ni  kati  ya  watoto  mapacha  waliozaliwa  jijini Mwanza  na mama  ambaye  jina lake  halikupatikana mara moja.

 
Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua  kumtoa mtoto mmoja kwa mama  mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea,  wakati huo mtoto  huyo alikuwa na miezi  mitatu.

Mama wa  Flora alikaa  na  mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye hadi  alipofikwa na janga hilo.
 
Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza  kufanya  kitendo  hicho  kwa sababu mkewe (Flora)  ameondoka  nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa kile  kilichodaiwa  kwamba kuna ugomvi  mkubwa ndani ya ndoa yao.
 
Taarifa  zaidi  zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo  nyumbani kwake huku mlalamikaji  akidaiwa  kuchukuliwa  na  familia ya Mchungaji Josephat Gwajima...
 
>>>GPL

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com