Bw. Amou Haji wa Tehran amesema wazi kuwa hana tatizo katika maisha yake ila anachohitaji kwa sasa ni mwanamke atakayempenda maishani.
Haji, mwenye umri wa miaka 80 hajawahi kuoga wala maji kugusa mwili wake kwa miaka 60 sasa.
Mwanaume huyu anayeishi mwenyewe katika kijiji cha Dejgah Kusini mwa Iran katika jimbo la Fars anaishi kwa kula nyama za vidungumaria..
Bwana Haji ameendelea kusema kuwa ameamua kuishi maisha haya ya upweke baada ya kupata matatizo ya kutengwa katika ujana wake. Lakini Haji ameendelea kusema japo kuwa amekuwa na maisha yasiyovutia kwa wakati wote huu bado anaimani kubwa kuwa atatokea mtu wakuujaza moyo wake na furaha.
Social Plugin