Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LEO KAMERA ZETU ZIMENASA HIKI MJINI SHINYANGA,TAZAMA PICHA

Hapa ni katika barabara ya Magadula,barabara inayotenganisha kata ya Ngokolo na kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga,ambako katika pitapita zake kamera za Malunde1 blog zimefanikiwa kumnasa mwandishi wa habari wa radio faraja ya Shinyanga Steve Kanyefu maarufu kwa jina la Mwanapori au bwana Michapo akiwa katika mihangaiko yake,hapa anangalia namna mitaro katika barabara hiyo imeshidwa kuhimili maji ya mvua matokeo yake kujikuta ukizalishwa mtaro usio rasmi na kuharibu barabara kama unavyoona hapo mbele


Kama unavyoona mbele ni mtaro usio rasmi uliovamia barabara na nyuma ni mtaro halisi ambao umeshindwa kuhimili maji ya mvua matokeo yake kubomoka.Barabara hiyo pindi mvua ikinyesha hugeuka mto

Mwandishi wa habari  Steve Kanyefu akiwa  ameshika kichwa akishangaa namna mtaro ulivyoharibika,hali ambayo husababisha barabara hiyo kugeuka mto mvua zinaponyesha

Mtaro katika barabara ya Magadula inayotenganisha kata ya Ndembezi na  Ngokolo mjini Shinyanga



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com