MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI,SHINYANGA YAFANYIKA UWANJA WA KAMBARAGE
Thursday, May 01, 2014
Ni katika viwanja vya CCM Kambarage mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani kimkoa.Wa tatu kutoka kulia ni mgeni rasmi katika sherehe hizo kaimu mkuu wa mkoa wa
Shinyanga Annarose Nyamubi ambaye ni mkuu wa wilaya ya
Shinyanga,akiwa katika jukwaa kuu wakati wa kupokea maandamano ya wafanyakazi kutoka mjini Shinyanga kuelekea katika uwanja wa Kambarage.Wa tatu kutoka kushoto ni mwenyekiti
wa shirikisho la wafanyakazi mkoa wa Shinyanga Fue Mlindoko.
Miongoni mwa mabango waliyokuwa wamebeba wafanyakazi wa mkoa wa Shinayanga leo katika uwanja wa ccm Kambarage mjini Shinyanga,ambapo pamoja na mambo mengine wafanyakazi hao wamewataka waaajiri kuacha tabia ya kuwanyanyasa na kuwafukuza kama wanyama,lakini pia kuitaka serikali kuwajali wafanyakazi kwa kusimamia sheria ya waajiriwa ya mwaka 2008 kuruhusu wafanyakazi wachague mifuko ya hifadhi ya jamii wanayoitaka mwenyewe bila kulazimishwa na waajiri waa kutokana na baadhi ya mifuko hiyo kushindwa kuwanufaisha wafanyakazi katika mafao yao kama unavyoona kwenye bango hilo hapo mbele. Picha kwa hisani ya Stella Ibengwe
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin