Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makubwa haya!!! JAMAA AJILIPUA MOTO KISA KAOTA KUMFUMANIA MKE WAKE AKIFANYA MAPENZI NA JIRANI YAKE


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Katoro Mkoani Geita Makelemo Daud (35) amejiunguza kwa moto mwili mzima baada ya kuota ndoto kuwa amemfumania mke wake akifanya tendo la ndoa na Jirani Yake. 


Makelemo amedai kuwa usiku wa kuamkia juzi akiwa amelala katika nyumba ya wageni iitwayo Choma Majani ya kijiji cha Bukombe wilayani Bukombe mkoani geita aliota ndoto wakati akitokea Nzega kuwa amemfumania mke wake.

Aliji funika godoro na kuliwasha moto ili kuepuka fedheha alizokuwa amezipata, amedai kuwa baada ya kuona maumivu makali alipiga kelele na wenye nyumba hiyo walikuja kumuokoa na hatimaye kumfikisha katik ahospitali ya wilayani Bukombe ambapo anahudumiwa hivi sasa .

Waandishi wa habari wamepiga hodi katika hospitali hiyo wodi namba tano na kumkuta mtu huyo makelemo akiwa ameungua mwili mzima huku akidai kuwa japokuwa ameungua mwili mzima lakini hali yake hivi sasa inaendelea vizuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com