Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Makubwa haya!! WALE WAUMINI WALIOLISHWA NYASI NA MCHUNGAJI WAO,SASA HIVI WAMEANZA KULA MITI

Dada aliyepona jino kwakutafuna majani akiendelea na lishe yake kwa furaha huku wenzake wakiwa wamelala. 

Ikiwa ni miezi miwili imepita toka huduma ya mtume Lesego Daniel wa nchini Afrika ya kusini ya Rabboni Ministries Centre kuwa maarufu duniani baada ya waumini wake kula manyasi ikiwa moja ya namna ambavyo roho mtakatifu alivyowaongoza, bado waumini wa huduma hiyo wanaendelea kula manyasi na kufanya njia moja wapo ya kupata uponyaji licha ya watu wengi kupinga ufunuo wa namna hiyo.
Kupitia picha zilizotolewa na huduma hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook, umeonyesha waumini wakikimbilia matawi ya miti na kuanza kula majani yake, huku mmoja wa waumini aliyefika kanisani hapo kwa mara ya kwanza amesema amepona jino lililokuwa likimuuma mara baada ya kula majani, amesema kwamba alifika kanisani hapo kwa mara ya kwanza siku ya ijumaa akiwa na dawa za kutuliza maumivu pamoja na panado lakini hazikumsaidia ila majani yalimponya na kwamba akirudi nyumbani mumewe (ambaye pia mtumishi) atafurahi sana kwa uponyaji huo.

Huduma hiyo ambayo inaongozwa na mtume msomi Lesego Daniel imekuwa ikipingwa na watu wengi hasa baada ya tukio la waumini kula nyasi huku pia mtume huyo mda mwingine huwafanyia maombi waumini wake huku akiwa amewakanyaga migongoni.

 Licha ya kelele kutoka kwa viongozi wa dini na makanisa mbalimbali kuwakataza waumini wao na wakristo kuwa makini na huduma ya mtumishi huyo, ndio kama wamewaruhusu kwenda huko kwakuwa inasemekana huduma hiyo imeendelea kujikusanyia waumini kila kukicha. Huduma hiyo ilikuwa ikifanya huduma zake katika majengo ya chuo kikuu cha teknolojia cha Tshwane kwasasa wamepata enero lao ambalo wameliita shamba la Rabboni ambalo wanatarajia kuhamia huko jumapili ijayo ya tarehe 4

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com