Karibia kila nyumba ina meza ya biashara mjini Shinyanga kama unavyoona pichani |
Biashara inaendelea |
Kushoto ni diwani wa kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga akizungumza leo wakati wa kikao cha kamati ya maendeleo ya kata yake,kulia kwake ni afisa mtendaji wa kata hiyo James Dogani.Pamoja na mambo mengine kikao hicho kiliazimia kupiga marufuku uwekaji wa meza za biashara nje ya nyumba kwani sasa karibia kila nyumba mfano katika kata hiyo kuna meza ya nyanya nje |
Wakazi wa kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga wameagizwa kuacha tabia ya kuweka meza za biashara mbalimbali za bidhaa za sokoni mbele ya nyumba zao badala yake wapeleke biashara zao katika soko la Ndembeze lililopo katika kata hiyo kwani kufanya vile ni kutowatendea haki wafanyabiashara walioko kwenye masoko.
Agizo hilo limetolewa leo na diwani wa kata ya Ndembezi ambaye pia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila wakati wa kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hiyo kilichofanyika katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo mjini Shinyanga.
Nkulila amewashauri wananchi wanaoweka /meza vibanda vya biashara kama vile nyanya na mchicha kupeleka bidhaa hizo kwenye masoko ili kuepuka malalamiko ya wafanyabiashara wengine wanaopeleka bidhaa zao kwenye masoko.
Nkulila alisema masoko mengi likiwemo la Ndembezi yamekuwa hayajai kutokana na baadhi ya watu kuanza kufanya biashara kwenye nyumba zao hali inayozuia malalamiko kwa wafanyabiashara walioko sokoni kwa vile wanatoa ushuru hapo sokoni.
Nkulila alitumia fursa hiyo kuwataka watu wanaomiliki maduka kuacha mara moja tabia ya kuuza bidhaa za sokoni kama mchicha na nyanya kwani vifaa kupelekwa sokoni huku akiwataka wafanyabiashara katika masoko kuzingatia suala la usafi ikiwemo kuepuka kuchoma taka ndani ya masoko.
Katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu vinavyoendelea mjini Shinyanga mfano wafanyabiashara kuvamiwa na majambazi,kikao hicho cha kamati ya maendeleo ya kata ya Ndembezi kiliazimia kukutana na wafanyabiashara wote katika kata hiyo siku chache zijazo ili kuwapa elimu kuhusu masuala ya ulinzi na usalama kikao ambacho kitahusisha pia maafisa kutoka jeshi la polisi.
Nao wajumbe wa kikao hicho waliomba kufanyika kwa usajili wa wakazi wa eneo hilo ili kuwabaini wakazi wake ili kudhibiti vitendo vya uhalifu huku wakisisitiza zoezi hilo kujikita kwa waendesha pikipiki na baiskeli ambao wanadaiwa kutumiwa na kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Aidha wajumbe hao walisema suala la ulinzi ni la jamii nzima hivyo kuitaka jamii kushiriki kikamilifu badala ya kuwaachia polisi peke yao huku wakitoa wito kwa akina mama kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa pale wanapohisi ama kuona uhalifu ukitendeka katika jamii.
Na Kadama Malunde wa Malunde1 Blog-Shinyanga