MAMLAKA YA MAPATO NCHINI (TRA) YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA KUHUSU MASHINE ZA EFDs
Friday, May 02, 2014
Awali meneja
wa TRA mkoa wa Shinyanga Ernest Dundee akifungua
mafunzo hayo ya siku moja kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika
ukumbi wa Karena Hoteli mjini Shinyanga alisema vyombo vya habari ni
kiunganishi muhimu kati ya TRA na wananchi ndiyo maaana wameandaa mafunzo kwao
ili kuwajengea uelewa zaidi kuhusu mashine za EFDs ili waweze kuandika habari
zao kwa usahihi zaidi.
Afisa mwandamizi Mkuu Elimu TRA Makao Makuu jijini
Dar es salaam Hamisi Lupenja akizungumza leo wakati wa mafunzo maalumu kwa
waandishi wa habari wa mkoa wa Shinyanga kuhusu matumizi ya mashine
za kodi za kutolea risiti (EFDS)iliyofanyika katika ukumbi wa Karena Hoteli
mjini Shinyanga.
Alisema Serikali iliamua kuanzisha mfumo wa utoaji risiti kwa
kutumia mashine za kodi (EFDs) 1 Julai,2010,ambapoawamu ya kwanza ni kwa wafanyabiashara waliosajiliwa
na VAT na awamu
ya pili ni kwa wafanyabiashara ambao
hawajasajiliwa na VAT.
Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo,ambapo Afisa mwandamizi mkuu elimu TRA Makao Makuu jijini
Dar es salaam Hamisi Lupenja aliongeza kuwa mfumo huo ulianza na wafanyabiashara wa VAT mwaka Julai, 2010 na mfumo wa pili ulizinduliwa
15/5/2014 na unahusu wale ambao hawajasajiliwa na VAT wenye mauzo yanayozidi
milioni 14.0 kwa mwaka na unaanza na wafanyabiashara 200,000.
Lupenja ambaye alikuwa mwezeshaji aliongeza kuwa
pamoja mashine hizo kuwa na faida kama
vile kutoa uhakika wa usalama
wa taarifa za biashara kwani taarifa hizo hutunzwa katika kifaa
maalumu(Fiscal memory)pia ni njia nzuri ya kupunguza ujanja na wizi unaoweza kufanywa na
wauzaji ambao si wenye mali lakini bado wafanyabiasharahawatumii
mashine hizo kwa sababu mbalimbali.
Aliyesimama ni bwana
Chibura Makorongo wa gazeti la Uhuru na Mzalendo akichangia mawili matatu
katika mafunzo hayo kwa waandishi wa habari.Katika mafunzo hayo mwezeshaji Lupenja aliziomba taasisi zote kufanya manunuzi kwa
wafanyabiashara wenye mashine za EFDs pamoja wananchi kujenga tabia ya kudai
risiti ili kuwa na uhakika na uhalali wa bidhaa zilizonunuliwa
na kuonyesha uzalendo kwa kuchangia katika maendeleo ya taifa.
Mwezeshaji huyo
alitumia fursa hiyo pia kubainisha aina tatu za mashine za kodi Rejesta za Kodi za Kielekitroniki (Electronic
Tax Register - ETR)ambapo
Rejesta hii hutumika kwa
wafanyabiashara wa rejareja, wanaotoa risiti kwa maandishi ya mkono na wale
ambao watakuwa wanauza bidhaa kwa kutembeza kwa wateja.
Alitaja aina ya
pili ni Printa za kosi za kielektroniki za Kodi (Electronic Fiscal Printer EFP)
ambapo alisema Mashine hii hutumika kwa wafanyabiashara wa rejareja ambao wanatumia mtandao wa kompyuta katika utoaji wa
risiti na ankara za madai na kwamba mashine hii hutumika hususani katika maduka makubwa (Supermarkets), Vituo
vya Mafuta (Petrol Stations) na
shughuli za ukataji wa risiti (Ticketing).
Alisema aina ya tatu ni Mashine za Alama za Kodi (Electronic
Signature Devise - ESD) ambapo alisema mashine hizi hutumika kwa
wafanyabiashara ambao hutumia programu
maalumu za biashara katika utoaji
wa risiti na ankara za madai na
kwamba Mashine hizi zina uwezo wa
kuratibu shughuli za kibiashara katika mtandao huo na kuifanya kompyuta
kutokuwa na uwezo wa kutunza (save) au kuchapa (print) taarifa yoyoye bila
idhini ya mashine yenyewe.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin