Mwili wa marehemu Frank ukitolewa ndani ya bwawa hili baada ya kupatikana-Picha na BICON PRODUCTION-KAHAMA |
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni wakati mtoto Frank akiogelea na wenzake katika Bwawa hilo lililopo maeneo ya KTM wilayani Kahama, ambapo alizama kusababisha kifo chake.
Mwili wa Marehemu Frank umefanikiwa kutolewa leo majira ya saa nne asubuhi, ukiwa chini ya kina kirefu katika bwawa hilo, mara baada ya hapo jana wazamiaji mbalimbali kuhangaika kuutafuta bila mafanikio yoyote.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu ambaye alikuwa akifanya kazi ya kuchunga mifugo, alifika katika bwawa hilo akiwa na Panga ambalo inasemekana alitumwa na mwajiri wake kukata majani kwa ajili ya kulisha mifugo hiyo.
Kwa mujibu wa Wachungaji wenzake, Marehemu Frank mara kwa mara amekuwa akiwatizama wenzake wakiogelea huku yeye akiogopa, lakini jana aliamua kuogelea kwa lengo la kujifunza kuogelea kama wenzake na matokeo yake akazama.
Muuguzi mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Kahama Richard Mabagala amethibitisha kupokea mwili wa marehemu leo asubuhi, na kwamba umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.
Jeshi la polisi wilaya ya kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba taratibu za Mazishi zinafanywa na Wazazi wa Marehemu ambao ni wakazi wa Busenda kata ya Kilago wilayani humo.
TAZAMA HAPA VIDEO UONE JINSI MWILI WA MAREHEMU FRANK FRED ULIVYOOPOLEWA MAJINI NA WAZAMIAJI HUKO KAHAMA
Social Plugin