MASKINI MUME NA MKE WANUSURIKA KUFA KWA KUUNGUA MOTO,TAZAMA PICHA ZINASIKITISHA,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI
الثلاثاء, مايو 27, 2014
Majeruhi wa kwanza Chacha Wambura (35)akiwa amelazwa katika wodi namba 7 katika wilaya ya Geita baada ya kuungua moto katika kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita mkoani Geita.
Majeruhi wa pili mke Chacha Wambura bi Happiness Chacha (22) akiwa amelazwa katika wodi namba 8 katika hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kuungua moto yeye na mme wake-Picha zote na Valence Robert
Wanandoa
wawili wakazi wa kijiji cha Lwamgasa wilayani
Geita mkoani Geita Happiness Chacha(22)
na mme wake Chacha wambura(35) wamenusurika kufa baada ya nyumba yao kuungua
moto katika kibanda chao cha bar.
Tukio
hilo limetokea jana usiku saa nane usiku katika kijiji cha Lwamgasa ambapo
kufuatia tukio hilo majeruhi wakikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Geita
mkoani Geita walipolazwa wodi namba 7 na 8.
Robina Isack anayewauguza amesema kuwa usiku huo
wa saa 8 waliona moto unawaka bila kujua umeanzia wapi huku wakishangaa kwa
vile hawatumii nishati hiyo ya umeme na wala hapakuwa na moto waliokuwa
wamewasha ndani.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Na Valence Robert wa
Malunde1 Blog -Geita
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin