Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Mauaji Kahama!! MAMA NA BINTI YAKE WAPIGWA RISASI WAKIPIKA CHAKULA CHA USIKU

Wanafamilia wawili mama na binti yake wameuawa kwa  kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakiwa nyumbanoi kwao jikoni wakiandaa chakula cha usiku katika kijiji cha Nyabusalu kata ya Bulungwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga .

Kamanda wa jeshi la  polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku.

Kamanda Mangalla amewataja waliouawa  kuwa ni Milembe Masanja(mama) ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kwenye kwapa la mkono wa kushoto na  Kulwa Madirisha(binti) ambaye  alipigwa risasi kidevuni na tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo.

Aidha kamanda Mangalla amesema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa na hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi huku na kwamba bunduki iliyotumika katika mauaji hayo inadhaniwa kuwa ni aina ya gobore kutokana na  majeraha waliyokutwa nayo marehemu.

 Na Kadama Malunde wa Malunde1 Blog -Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com