Wanafamilia wawili mama na binti yake wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakiwa nyumbanoi kwao jikoni wakiandaa chakula cha usiku katika kijiji cha Nyabusalu kata ya Bulungwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga .
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku.
Kamanda Mangalla amewataja waliouawa kuwa ni Milembe Masanja(mama) ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi kwenye kwapa la mkono wa kushoto na Kulwa Madirisha(binti) ambaye alipigwa risasi kidevuni na tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo.
Aidha kamanda Mangalla amesema chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa na hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi huku na kwamba bunduki iliyotumika katika mauaji hayo inadhaniwa kuwa ni aina ya gobore kutokana na majeraha waliyokutwa nayo marehemu.
Na Kadama Malunde wa Malunde1 Blog -Shinyanga
Social Plugin