Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya |
Kijana
mmoja aliyejulikana kwa jina la Mihangwa
Maguta (30) mkazi wa kijiji cha Nyenze Matelu kata ya Mwadu- Luhumbo tarafa ya
Mondo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ameuawa baada ya kupigwa kwa jiwe
kubwa kichwani na watu anaodaiwa kuwadhulumu pesa za mauzo ya madini ya almasi.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na kaimu kamanda wa jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya tukio hilo limetokea jana (Mei
7,2014) saa moja asubuhi katika kijiji hicho cha Nyenze Matelu wilayani Kishapu.
Imedaiwa
chanzo cha mauaji hayo inasadikiwa kuwa marehemu amewadhulumu wenzake watatu pesa za mauzo ya madini ya
almasi.
Tayari
jeshi la polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watuhumiwa wa mauaji hayo
akiwemo Makoye Manyenze aliyesababisha kifo cha Mihangwa Maguta.
Watuhumiwa
wengine wanaoshikiliwa na polisi ni Abdalah Idd (32) na Ally Omary (22) wote
wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Nyenze
Matelu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Social Plugin