Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ALBINO AUAWA KIKATILI KWA KUKATWA KATWA MAPANGA VIUNGO VYAKE,WAUAJI WATOWEKA NA VIUNGO VYAKE

albinoo2

Mwanamke mmoja Mughu Lugata (40) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) mkazi wa kijiji cha Gasuma kata ya Nkololo wilayani bariadi mkoani Simiyu ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ambao wametoweka na viungo vyake .

Kamanda wa polisi mkoani wa Simiyu Charles Mkumbo amesema tukio hilo limetokea  usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa marehemu, ambapo wahusika wa mauaji baada ya kufanya mauaji hayo walimkata mguu wake wa kushoto, sehemu ya goti, vidole 2 vya  mkono wa kushoto pamoja ukucha wa kidole gumba kisha kutoweka navyo.

Chanzo cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni imani za kishirikina na kwamba
tayari watu wawili ambao ni waganga wa kienyeji  wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com