Mwanamke mmoja Mughu Lugata (40) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) mkazi wa kijiji cha Gasuma kata ya Nkololo wilayani bariadi mkoani Simiyu ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana ambao wametoweka na viungo vyake .
Kamanda wa polisi mkoani wa Simiyu Charles Mkumbo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana nyumbani kwa marehemu, ambapo wahusika wa mauaji baada ya kufanya mauaji hayo walimkata mguu wake wa kushoto, sehemu ya goti, vidole 2 vya mkono wa kushoto pamoja ukucha wa kidole gumba kisha kutoweka navyo.
Chanzo cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni imani za kishirikina na kwamba
tayari watu wawili ambao ni waganga wa kienyeji wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.
Social Plugin