Utafiti huo umekuja baada ya kubainika kuwa ugonjwa wa kupooza umezidi kushika kasi hasa kwa mataifa ambayo yana watu wenye vipato vikubwa.
Wataalamu walioshiriki katika utafiti huo walieleza kuwa vitamin zilizopo kwenye matunda na mboga za majani zina uwezo mkubwa wa kumwondoa mlaji kwenye hatari ya kupooza.
“Inaweza kuonekana ni kitu cha ajabu lakini ndiyo ukweli ulaji wa matunda na mboga za majani ni kinga ya asili ambayo inaweza kumwondoa binadamu katika hatari ya kupooza,” alisema Dk John Baden.
Utafiti huo unaenda sanjari na ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo inaeleza kuwa ulaji wa matunda na mboga za majani unaweza kupunguza kasi ya ugonjwa huo kwa asilimia 19.
Nchini China ugonjwa wa kupooza unatajwa kusababisha vifo vya watu wengi kuliko magonjwa mengine.
Na Elizabeth Edward