Meya mwenye utata wa mji wa Toronto,Rob Ford amesema kuwa atachukua mapumziko ya muda ili kutatua tatizo lake la ulevi
Mwanasheria wa Meya huyo Dennis Morris amesema mteja wake anaelewa kuwa ana tatizo linalomdhalilisha na anataka kuchukua hatua kulitatua.
Tangazo lake linajiri wakati ambapo
magazeti mawili ya Canada yanasema yamepata kanda mpya ya video yenye
kutia aibu ya Bwana Ford.
"Mwaka
uliopita Meya Rob Ford alikiri kuwa alikuwa akitumia mihadarati akiwa
meya baada ya kukataa kwa miezi kadhaa kuvuta midarati hiyo wakati
anapolewa ambapo pia alipinga wito wa kumtaka ajiuzulu."
Katika kanda hizo Bwana Ford anaonekana akitumia
mihadarati aina ya cocaine akiwa amelewa chakari huku nyengine
akionekana akitoa matamshi mabaya kuhusu wanawake na wanasiasa wenzake
katika baa moja.
Mkanda huo wa video unamwonyesha katika miezi ya hivi karibuni akiwa amelewa.
Mwaka uliopita Bwana Ford alikiri kuwa alikuwa
akitumia mihadarati akiwa meya baada ya kukataa kwa miezi kadhaa kuvuta
midarati hiyo wakati anapolewa ambapo pia alipinga wito wa kumtaka
ajiuzulu.
Pia polisi wana malalamiko kwa njia ya maandishi
kuwa meya huyo amekuwa akituhumiwa akitumia lugha ya matusi,
akiwatishia wafanyakazi wenzake, akiwadhalilisha wanawake na kutumia
mihadarati akiwa kwenye mgahawa. Tuhuma ambazo meya huyo amezikana.
Meya huyo sasa anataka kugombea tena nafasi hiyo
mnamo mwezo Octoba,lakini anasema kwamba atapumzika kwa muda katika
kampeni zake za umeya ili kutatua tatizo lake la ulevi.
via>>bbc
Social Plugin