Michepuko Noumaa!! JAMAA AJINYONGA KISA KUTAMKIWA NA MKEWE KUWA WATOTO ANAOWALEA SIYO WA KWAKE


Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Antony Komba(30) mkazi wa mtaa wa Tambuka reli mjini Geita amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kujining'iniza katika mti wa mpera kwa kile kilichotajwa kulea watoto wasio wa kwake.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea usiku wa kuamkia leo
ambapo Antony Komba amekutwa amenyonga juu ya mti wa mpera baada ya kutamkiwa na mke wake Vumilia Msomi(29) wakati wa ugomvi wa kifamilia  kuwa watoto watatu aliyezaa naye siyo wa kwake bali ni wa mwanamme mwingine

Wamesema kabla ya kifo chake,jana marehemu alikuwa na ugomvi na mkewe Vumilia Msomi juu ya watoto wao watatu mapacha ambao ni Johnson, Joel na Jonathan wenye umri wa miezi 9,waliowazalia katika hospitali ya Tumbi mkoani pwani kabla wanandoa hao hawajahamia mkoani Geita kwa wazazi mwanamke wa Vumilia Msomi.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo shemeji wa marehemu Pendo Msomi amesema kuwa shemeji yake (Antony Komba) baada ya ugomvi na mkewe alienda kulala na ilipofika saa 2 usiku  marehemu aliondoka kwenda kuangalia mpira kwa vile ilikuwa kawaida yake.
Hata hivyo tofauti na ilivyo kawaida ya kwenda kuangalia mpira na kurudi usiku, jana hakuweza kurudi na ndipo alipokutwa amejinyonga hadi kufa kwenye mti wa mpera.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa marehemu aliandika barua ya kuzungumzia historia ya maisha yake tangu alipomuoa mwanamke huyo na jinsi alivyofikia hatua ya kumsaliti kwa watoto hao.

Kamanda Konyo amesema katika barua hiyo marehemu ameeleza jinsi alivyohangaika  kumhudumia mwanamke huyo kipindi akiwa mimba matokeo yake anamsaliti kwa kuzaa na mwanamme mwingine.
Hadi sasa jeshi la polisi linamsaka mke wa marehemu ambaye amefanikiwa kuzaa naye watoto watano,anaedaiwa kusababisha kifo cha mme wake ambaye amekimbia na hajulikani alipo.

 Na Valence Robert wa Malunde1 Blog-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم