Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Annarose Nyamubi-Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 Blog |
Mifuko ya hifadhi ya jamii nchini imetahadharishwa kuacha kufanya kazi kwa kutapeli watumishi wapya wa serikali hususani waajiriwa wapya kwa kutoa fomu ambazo zimeshajazwa bila kutoa ushauri mzuri, hali ambayo inasababisha baada ya muda wateja wao kujutia kujiunga na mifuko hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi kwenye semina ya elimu juu ya hifadhi ya jamii kwa viongozi wa serikali mkoa wa Shinyanga,iliyoandaliwa na mamlaka ya usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA).
Mkuu huyo wa wilaya alisema baadhi ya mifuko haifanyi kazi zake kwa uwazi hivyo kuwatapeli watumishi hasa waajiriwa wapya ambao wanakuwa hawaifahamu vizuri.
Mkuu huyo wa wilaya alisema baadhi ya mifuko haifanyi kazi zake kwa uwazi hivyo kuwatapeli watumishi hasa waajiriwa wapya ambao wanakuwa hawaifahamu vizuri.
Mkuu wa wilaya aliitaka mifuko hiyo kufanya kazi zake kwa uwazi na kutoa huduma ili yobora kwa wateja wao ili kuwahamasisha watumishi wengine kutoka serikalini,,mashirika,,taasisi na watu binafsi kujiunga ili kujiwekea akiba ya uzeeni pamoja na mafao mengine ukiwemo uzazi na matibabu .
“ Inaumiza pale ambapo unawekeza baada ya miaka mitano halafu kiwango cha pesa unazopata,kije kufanana na mtu aliyewekeza leo wakati gharama za maisha zinapanda kila kukicha,ninawaomba ndugu zangu mnaosimamia mifuko hii kwenda na mabadiliko ya hali halisi iliyopo”alisema Nyamubi.
Nyamubi alisema mfuko wa hifadhi ya jamii(NSSF) umekuwa ukilalamikiwa na watumishi wengi kwa kushindwa kuboresha huduma zake, hali ambayo alisema inaweza kusababisha kukosa wanachama na malengo yao kutofikiwa na kutolea mfano wakati wa mei mosi mabango mengi yalikuwa yaki ulenga mfuko huo kwa kuumiza watumishi katika mafao.
Siku ya Mei Mosi Shinyanga -Picha kutoka maktaba ya Malunde 1 blog |
Katika hatua nyingine Nyamubi alisema mifuko hiyo inatija kubwa iwapo jamii itaitumia vizuri katika kujiletea maendeleo na kuweka akiba ya uzeeni,ambapo yote hayo yatafanikiwa kwa kufanyakazi kwa uwazi na kuboresha huduma wanazozitoa .
Kwa upande wake mwezeshaji wa semina hiyo kutoka (SSRA) Dar es salaam Mohamed Nyasama,alisema mpaka sasa ni 4.5 ya watanzania wote ndiyo wamejiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii,idadi ambayo bado iko chini na kuwataka watanzania kubadilika na kuwekeza kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuwa ni mkombozi wa kweli.
Alisema mamlaka hiyo inafanya kazi ya kutetea na kulinda maslahi ya wanachama,wafanyakazi na wastaafu ili kuleta faida kwa wateja kwa kuboresha uhakika wa maisha yao ya baadaye,kinga dhidi ya majanga kwa watanzania na kukuza uwekezaji nchini.
Naye katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi alisema utendaji mbovu wa baadhi ya mifuko unakatisha tamaa watumishi kujiunga na mifuko yao, kutokana na kuona hali halisi jinsi wazee wastaafu wanavyohangaika kufuatilia mafao yao wakati takwimu zote zipo lakini kwenye malipo inakuwa tatizo.
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi mkoa wa Shinyanga (TUCTA)Fue Mlindoko,alisema kero kubwa wanazokumbana nazo ni mafao kutokuwa sawa miongoni mwa watumishi wakati wakitambua fika tarehe za kuajiriwa na kustaafu, lakini cha kusikitisha wakati wa kuchukuwa mafao yanakuwa kidogo kinyume na matarajio yao.
Stori na Stella blog
Social Plugin