Mwanafunzi wa darasa la tatu Sofia
Damasi (12) wa shule ya msingi Lutozo katika kata ya Katoro wilayani Geita mkoani
Geita amelazwa katika kituo cha afya mjini Katoro baada ya kuchomwa moto
sehemu mbalimbali za mwili wake na bibi yake.
Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 8
katika kitongoji cha Bulengahasi.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa
bibi huyo anayeitwa Monica Petro(50) ambaye ni mkazi wa Katoro aliamua kuchukua
uamuzi huo baada ya mjukuu wake huyo kumwibia karanga za mbegu alizokuwa
amezitunza kwa ajili ya kupanda.
Akiongea kwa shida alikolazwa wodi ya
wanawake mtoto huyo amesema kuwa alikumbwa na mkasa huo juzi majira ya saa 8
mchana muda mfupi baada ya kumaliza kula chakula cha mchana.
“Baada ya kumaliza kula chakula bibi yangu
alitoka nikabaki mimi nyumbani na baba zangu wadogo wawili ambao nao baadaye
waliondoka na kwenda kazini kwao na ndipo bibi yangu alirudi tena na kuingia
jikoni’’,alieleza.
“Bibi alipoingia jikoni aliniita jikoni na
nilipoenda jikoni bibi yangu alifunga mlango kwa ndani na kisha kunifunga kamba
aina ya mpira mikononi mwangu na kuanza kunitesa’’alifafanua mtoto huyo/
Alisema mara baada ya kufanya unyama huo
bibi yake alitoka nje na kumfungia ndani na ndipo alipoanza kupiga kelele za
kuomba msaada ndipo majirani walifika na kumfungulia mlango na kamba hiyo na
baada ya hapo walimpeleka kituo cha polisi na kupewa hati namba tatu ya
matibabu(PF3) kwa ajili ya kupata matibabu na kisha kupelekwa kituo cha afya
cha Katoro.
Afisa mtendaji wa kata
ya katoroAloyce Kamuli alipoulizwa juu ya tukio hilo alisema hana taarifa kuhusu tukio hilo.
Na Valence Robert-wa
Malunde1 blog Geita
Social Plugin