MUONGOZAJI WA BONGO MOVIES AFARIKI DUNIA GHAFLA BAADA YA KUANGUKA CHINI AKIWA KAZINI



 


Adam Kuambiana enzi za uhai wake
 

Chanzo cha habari kimeripoti kwamba msanii Adam Phillip Kuambiana ambaye ni mwongozaji,muigizaji na mwandishi wa sinema amefariki leo muda mchache uliopita baada ya kuanguka ghafla wakati akiwa location akiwajibika katika shughuli zake za sanaa na kuwahishwa haraka katika hospitali ya Maria Stopas iliyoko Sinza Afrika Sana jijini Dar es Salaam.


Rais wa shirikisho la filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifamba amethibitisha kutokea kwa msiba huo.



    Hizi ni baadhi tu ya kazi zake njema:
    Danija 
    Faith More Fire|
    Bad Luck
    Scola 
    The Boss 
    Mr.Nobody 
    Radhi ya Mke
    Lost Sons 
    Chaguo Langu 
    My Fiance 
    Jesica
    Life of Sandra 
    Basilisa
    My Flower 
    Regina
    Born Again 
    Its Too Late 
    Fake Pastors

Taarifa kamili kuhusu msiba wa producer Kuambiana itakuijia hivi punde........

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post