Mkazi wa Majengo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga Sophia Hamis(39) amefariki dunia kwa kujinyonga akiwa chumbani Kwake mjini Kahama.
Mtoto wa Kaka wa Marehemu Sophia aliyejitambulisha kwa majina ya Musa Alex amesema shangazi yake Marehemu Sophia kabla ya mauti kumfika juzi jioni; alikuwa anasumbuliwa na malaria hivyo jioni hiyo alikuwa amepumzika chumbani kwake.
Baada ya muda mrefu kupita Alex aliamua kumwita shangazi yake kwa ajili ya kumeza dawa ndipo alipogundua kuwa haitikii na baada ya kuingia chumbani alimkuta amekwishajinyoga kwa kutumia nguo ya kitenge na mwili umening’inia darini.
Jeshi la polisi wilayani humo lilifika katika eneo la tukio na kuupeleka mwili wa marehemu Sophia katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya wilaya ya Kahama huku upelelezi wa chanzo cha tukio hilo ukiwa unaendelea.
Na Marco Mipawa -Kahama
Social Plugin