Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMKE AMTETEA MME WAKE MAHAKAMANI ALIYETEKA KISHA KUBAKA MWANAFUNZI NA WANAWAKE WATATU


Thompson kushoto akiwa naAdriana wakiwa ufukweni.
Thompson akiwa na Adrian Ford siku ya harusi yao

Mwanamke mmoja, Adriana Ford-Thompson ambaye ni mhitimu katika chuo kikuu cha Cambridge amejitokeza na kumtetea mumewe, Mark Thompson kwa kosa la kuwavamia wanawake watatu na kufanya nao mapenzi kinguvu huko jijini London nchini Uingereza

Adriana 37,alikutana kwa mara ya kwanza na Thompson nchini Tanzania mwaka 2006 wakiwa katika utafiti wa misitu aliwaambiwa majaji kuwa bado anampenda mumewe huyo na kwamba ni mtu mwema na mkarimu  licha ya kupatikana kwa kosa la kuteka, kumbaka mwanafunzi na kuwashambuliwa wanawake watatu kwa kufanya nao mapenzi kinguvu.

Adrian ambaye kwa sasa ni mtafiti wa mazingira na mwalimu katika chuo York alimwambia jaji kuwa mara nyingi alipokuwa akienda ofisini alikuwa akimuacha mumewe nyumbani na pia hakujua kama kuna mwanafunzi wa chuoni hapo anapofanyia kazi kama alifanyiwa kitendo cha ubakaji na mumewe.

 Baada ya majaji kumhukumu kifungo cha maisha miaka 11 jela mumewe huyo kwa makosa nane ya ubakaji na utekaji kwa wanawake, mkewe alisikika akisema;

“Thompson ni mtu mkarimu sana, mwema na matanashati, nimemfahamu miaka kumi iliyopita ni zaidi ya rafiki yangu wa karibu, nitakuwa pamoja naye kwa kila kitu japokuwa atakuwa mbali na mimi lakini naamini aliyotenda ni kwasababu hakupata alichostahili.

Thompson ambaye pia ni mtoto wa mchungaji alijitetea kwa kusema kuwa hakuwahi kufanya mapenzi na mke wake na ndio sababu iliyopelekea kubaka wanawake hao.

Thompson alitokea Jamaica kwenda kuishi nchini Uingereza akiwa na umri wa miaka 16 ambapo alikuwa mwana karate kabla ya mwaka 2006 kuelekea nchini Tanzania kwa ajili ya kufanya utafiti wa misitu.

Alikutana na Adriana nchini Tanzania na mwaka 2007 walirudi Uingereza ambapo walifunga ndoa mwaka 2009.

CHANZO NI DAILYMAIL

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com