Mwanamke mmoja ameuawa kikatili kwa kukatwa katwa na mapanga sehemu mbalimbali za Mwili wake kwa kudhaniwa kuwa ana imani za Kishirikina.
Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Lushiku Tenganija Sono Msukuma aliyekuwa na Umri wa Miaka 59 wa kitongoji cha Senga kata ya Bugando Mkoani Geita ameuawa na mwili kuonekana muda wa Saa moja asubuhi ya leo ukiwa kwenye barabara ya mtaa umbali wa mita kama mia tatu kutoka nyumbani alipokuwa akiishi Marehemu pamoja na wajukuu zake watatu.
Marehemu amekatwa shingo kabisa na kutenganishwa na Mwili, mkono wa kushoto na kulia pamoja na bega la kulia.
Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bwana Joel Saanane (42) amethibitisha kutokea kwa Tukio hilo na kudai kuwa msako mkali unaendelea dhidi ya wauaji hao.
Social Plugin