MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA MAWE MAHAKAMANI NA NDUGU ZAKE

Mamake Farzana akiomboleza kifo cha mwanawe

Mwanamke mmoja nchini Pakistan amepigwa mawe na familia yake wakiwemo babake na ndugu zake wa kiume hadi kufariki. 

Aliuawa nje ya jengo la mahakama mjini Lahore.

Mwanamke huyo aliuawa kwa kuolewa na mtu ambaye alikuwa chaguo lake mwenyewe.

Farzana Bibi, mwenye umri wa miaka 31, aliolewa na Muhammad Iqbal miezi michache iliyopita bila ya idhini ya familia yake.

Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alishambuliwa na familia yake.

Kaka zake na binamu yake mmoja walimshika alipokuwa akiingia mahakamani na kuanza kumpigwa kwa mawe . Alifariki popo hapo.

Waliomuua walikimbia kabla ya polisi kufika katika eneo hilo.

Babake msichana huyo amekamatwa ingawa washukiwa wengine wangali hawajulikani waliko.

Kwa wanawake wanaoolewa na wapenzi ambao ni chaguo lao wenyewe, ni kitendo kisichokubalika kitamaduni katika baadhi ya maeneo ya Pakistan.

Mamia ya wasichana huuawa kwa kisingizio cha kuolewa na watu wasiokubalika na familia zao kila mwaka.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wanaamini kuwa kwa kuwa mauaji hayo hufanywa na familia zenyewe, huwa ni vigumu kufikisha kesi hizo kortini.
via>>bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم