mwanamke aitwaye Mariam Kidesheni(60) mkazi wa kijiji cha Isamilo kata ya Kamhanga wilayani Geita ameuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa mapanga.
Tukio hilo limetokea Me 25 mwaka huu saa 2 usiku ambapo inadaiwa kuwa mama huyo baada ya kumaliza kula chakula cha usiku alivamiwa na watu wasiofahamika
wakiwa na mapanga kisha kuanza kumkata kata sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kichwani,shingoni na sikioni hadi kufa.
Diwani wa kata ya Kamhanga Dionizi Bugali na Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Na Valence Robert wa Malunde1 blog-Geita
Social Plugin