Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA AFYA ALIELEZA BUNGE JINSI SERIKALI ILIVYOJIPANGA KUKABILIANA NA HOMA YA DENGUE

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Kebwe Stephen Kebwe amelieleza Bunge kuwa Wizara imeandaa mpango wa kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya Dengue uliosababisha vifo vya watu watatu kuanzia Januari mpaka mwezi huu ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ugonjwa huo. 

Mheshimiwa Kebwa amesema tangu ugonjwa huo ugundulike nchini, wagonjwa waliothibishwa kuugua ugonjwa huo ni 450 na kati ya hao wagonjwa wapya 60 wamegundulika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Pamoja na jitihada mbalimbali za serikali za kupambana na ugonjwa huo kama kutoa elimu kwa wananchi Timu ya Taifa ya maafa kukutana mara mbili kwa wiki ili kutathimini mikakati ya dharura naibu waziri huyo amewataka watanzania kutokuwa na hofu,kwani auambukizwi kwa kumuhudumia mgonjwa au kumugusa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com