News Alert!! TAARIFA KAMILI KUHUSU UGONJWA HATARI WA KUPIGWA MIHURI YA AJABU MWILINI YENYE SIKU ZA KUFA HUKO KAGERA,TAYARI UMEUA MTOTO



Habari kutoka kata ya Mutukula wilaya ya Missenyi mkoani Kagera nchini Tanzania zinaarifu kuwa kuna ugonjwa wa ajabu ulioanzia nchini Uganda na kuua watu wengi. 

Kwa mujibu wa habari kutoka Mutukula zinasema kuwa mtu hupigwa chata kwenye mwili wake ikionesha namba na baada ya siku zinazofanana za chata hiyo aliyepigwa chata hiyo(mhuri) huaga dunia.

Imeelezwa kuwa mtu hujikuta ana mhuri wa namba katika mwili wake  na hufariki dunia baada ya siku za namba hiyo ya mhuri iliyopo katika mwili wake ambayo hupigwa bila kujijua.

Tayari jana 13.05.2014 katika kitongoji cha Nyakera kata ya Mutukula wilayani Missenyi mtoto mwenye umri wa miaka minne (4) aitwaye Elizabeth Nantale amefariki dunia baada ya kupigwa mhuri wa namba 3 mgongoni na baada ya siku tatu kuisha akafariki dunia. 


Baba mzazi wa mtoto huyo bwana Isack Kayemba amethibitisha kutokea tukio hilo na kuongeza kuwa mtoto wake amefariki baada ya kuisha siku tatu alizoandikwa mgongoni. 

Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Nyakera Vedastus  Jonathan  Haruna amesema mtu akipata ugonjwa huo akipelekwa hospitali hawezi kupona labda aombewe kwani kuna baadhi ya watu wameombewa wakapona huko Uganda na kwamba mhuri hupigwa kwenye sehemu yoyote ya mwili mfano kwenye mkono,mgongoni,mguuni n.k

Amesema mpaka sasa jamii imepigwa na butwa kuhusu ugonjwa huo wa aina yake na kujikuta wananchi wakijawa na hofu kuhusu ugonjwa huo ambao unadaiwa umetokea nchini Uganda.

Ametumia fursa kuwataka wananchi kukagua watoto wao na wao wenyewe na pindi inapobaika mtu ana alama kwenye mwili wake basi afanyiwe maombi haraka iwezekanavyo.

Hata hivyo viongozi wa serikali bado hawajathibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo ambapo afisa mtendaji wa kata ya Mtukula amekanusha kuwepo kwa taarifa hizo na kuwataka wananchi kuacha kuwa na imani za kishirikina

Mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanari mstaafu Issa Njiku alipoulizwa juu ya tukio hilo amesema hajapata taarifa hizo. 


Tayari kuna mtu mwingine eneo hilo ana mhuri wa namba 14 kwenye mwili wake. 

Na Respicious John-Mutukula

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post