PICHA-- KINACHOENDELEA MSIBA WA MSANII WA BONGO MOVIE RACHEL HAULE

Rachel Haule enzi za uhai wake.
Wasanii wa Bongo Movies Unity wakiwa katika Viwanja vya Leaders kupanga mikakati ya msiba wa mwenzao, Rachel Haule ‘Recho’ aliyeaga dunia usiku  wa  kuamkia  leo baada ya kujifungua katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam
leaders1

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies wakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya taarifa za msiba wa msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' mapema leo kabla hawajakutana leaders club.
Mume wa marehemu Recho, George Saguda,akiwa na simanzi nzito kufuatia kifo cha mkewe.

Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule ‘Recho’ amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam imethibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere.

Taarifa zinasema Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم