Mkazi wa Kijiji cha Ibindi, Tarafa ya Nsimbo, wilayani Mlele, Michael Silanda (26), amefariki dunia baada ya kunywa pombe za viroba aina ya Zed kupita kiasi bila kula.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema tukio hilo lilitokea Mei 5 mwaka huu, saa 6 usiku kijijini hapo.
Alisema siku ya tukio, Silanda alikwenda baa na kuanza kunywa pombe hiyo bila kula kitu chochote hadi saa 6 usiku alipoamua kurudi nyumbani kwake huku akiwa amelewa kupita kiasi.
“Baada ya kufika nyumbani kwake aliingia ndani na kulala bila kula na siku iliyofuata saa 2 asubuhi ndipo walipomkuta akiwa amefariki dunia,” alisema.
Kamanda Kidavashari alisema uchunguzi wa awali umebaini kifo hicho kimesababishwa na Silanda kunywa pombe kupita kiasi bila kula chakula.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa kufanyiwa uchunguzi na utakapokamilika watakabidhiwa ndugu kwa mazishi.
Na Walter Mnguluchuma
Social Plugin