RAIS BANDA AAGIZA KUSITISHWA MARA MOJA KUHESABU KURA NA KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU

Baadhi ya viongozi wanaowania urais nchini Malawi
Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ulifanyika jumanne iliyopita.
Akizungumza Ikulu mjini Lilongwe muda mfupi uliopita ameiamuru Tume ya uchanguzi MEC kusitisha shughuli hiyo na kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe ndani ya siku 90 kutoka leo na kwamba yeye hatogombea tena urais wa nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji kura,kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya nchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post