Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu |
Ikiwa ni siku chache baada ya OCD wa wilaya ya Geita Busee Bwire kuangusha gari la polisi wilayani Geita lenye namba za uasjili PT 1998 na watuhumiwa 6 kukimbia kati ya wanane aliokuwa amewabeba kwenye gari hilo, baadhi ya wananchi wamemuomba waziri wa mambo ya ndani kuchukua hatua dhidi ya ocd huyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana baadhi ya wananchi wenye kutaka maendeleo na mkoa wa Geita wamesema kitendo cha OCD huyo kuendesha Gari mwenyewe wakati dereva wake alikuwepo ni kitendo kiovu japokuwa kamanda alisema alikuwa na leseni.
Pamoja na OCD huyo kuwa na matukio mengi yakiwemo ya kuachia watuhumiwa wa mauaji, kuangusha Gari la serikali na kuendesha kituo kwa ubabe pia anatuhumiwa kutembeza bakuri kwa ajili ya mchango wa kutengeneza Gari la polisi aliloharibu kwa wakuu wa vituo wote wa wilaya nzima ya Geita ili arudishe gharama zake za matengenezo kwa vile aligharimia kutoka mfukoni mwake.
Mwananchi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa ajili ya usalama wake alisema kuwa OCD huyo amekuwa ni kero kubwa kwa wananchi na askari wamekuwa wakimlalamikia sana kwa lugha za kuwatisha kuwa yeye ametoka Darfur nchini Sudan.
"Mimi kama mwananchi namshangaa OCD huyu, ni nani na analindwa na nani na amekuwa kero kubwa kwetu na kwa askari wake namuomba waziri mhusika kumchukulia hatua huyu ocd"alisema mwananchi huyo.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii umebaini kuwa pamoja na OCD Bwire kuangusha Gari hilo lilikwenda kutengenezwa kwenye Gereji bubu na huku likitengenezwa usiku na mchana lakini cha kushangaza Gari hilo halikufuata taratibu za serikari huku gari hilo likiwa limepasuka kioo cha mbele na kubanduka rangi.
Pamoja na uchunguzi huo mwandishi huyu umebainisha kuwa Gari hilo halikukaguliwa wakati linatoka Garage bubu hiyo pamoja na kuanza kazi mda huu huku baadhi ya askali polisi kulikimbia kulitumia kwa kuwa hawana imani na hilo Gari kwani halijulikani kama limekuwa imara kama lilivyo kuwa mwanzo huku ikisemekana kwamba mara baada ya kuanguka Injini ilishtuka na kuregea.
OCD Bwire aliangusha Gari la serikali na mei7 saa 2 usiku katika kijiji cha Bufunda alikokwenda kuwafuata watuhumiwa wa makosa ya jinai na kusababisha wahumiwa 6 kutoroka kati ya 8 alikuwa nao ndani ya gari hilo ambao ni Wiliam Michael,Charles Julius, Mussa Mashili,Joseph John, Nelson Rafael na Omari Sued huku askari aliyejulikana kwa Konsetebo Linusi wa kituo cha Nyarugusu kujeruhiwa baada ya meno yake mawili ya mbele kung’oka na kulazwa katika hospitali ya wilaya Geita.
Na baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari juu ya ajali hiyo OCD Bwire alisema kuwa yeye siyo msemaji wa jambo hilo na msemaji ni kamanda wa polisi mkoa ndio atalitolea maelezo.
Na Valence Robert-Geita