SSRA YATOA ELIMU KWA WATUMISHI WA JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA

Watumishi kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwenye ukumbi wa Ibanza hotel mjini  Shinyanga jana wakati wa semina ya siku moja kwa watumishi wa jeshi hilo iliyoandaliwa na SSRA,ikilenga kutoa elimu juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na kuitambulisha mamlaka hiyo ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Awali kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kihenya Kihenya akifungua semina ya siku moja kwa watumishi wa jeshi hilo iliyoandaliwa na SSRA,ikilenga kutoa elimu juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na kuitambulisha mamlaka hiyo ambayo ndiyo msimamizi mkuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
Mwanasheria mwandamizi wa mamlaka ya usimamizi wa sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii (SSRA) Salma Maghimbi kutoka makao makuu jijini Dar es salaam,akizungumza na watumishi kutoka jeshi la pilisi mkoa wa Shinyanga kwenye ukumbi wa Ibanza hotel manispaa ya Shinyanga.
Mwanasheria huyo aliwataka askari na watumishi wengine kuhakikisha wanafanya utafiti wa kina kabla ya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kwa sasa sheria imefanyiwa marekebisho hivyo wanaruhusiwa kuchagua mfuko wanaoutaka.
  
Watumishi wa jeshi la polisi mkoa wa shinyanga wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na mwanasheria mwandamizi juu ya mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na haki zao katika mifuko hiyo.
Afisa mfawidhi wa mfuko wa pensheni wa PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga,akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa semina ya mifuko ya hifadhi ya jamii juu ya mikopo kwa wanachama,ambapo alisema mikopo inayotolewa PSPF ni ya nyumba kwa watumishi hatua hiyo inatokana na kuona hitaji kubwa ni kupata nyumba kupitia mafao yao.
 
 

Pc -Rose kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga akichangia mawaili matatu wakati wa semina ambapo pamoja na mambo mengine alihoji kwa nini jeshi la polisi lisiwe na mfuko mmoja tu wa hifadhi ya jamii badala ya kutumia mifuko mbalimbali.

Meneja wa mkoa mfuko wa taifa wa bima ya afya Immanuel Amani akiwataka watumishi hao kutumia huduma za bima ili kurahisisha gharama za matibabu ambazo kwa sasa zinazidi kupanda .
  
                                          PICHA ZOTE NA STELLA BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم