RECHO: Hapa ndipo atakapo anza siku yake ya kwanza leo kwenye makazi yake mapya mbinguni. Shimo dogo ni kaburi la mtoto wake aliyefariki muda mfupi baada ya kumzaa katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam!
RECHO: KUZALIWA 1988 KUFARIKI: 2014. UMRI:miaka 26
Mwili wa marehemu Recho aliyekuwa msanii wa bongo muvi na mwili wa mtoto wake kwa sasa unatolewa katika hospitali ya taifa muhimbili na kupelekwa nyumbani kwao Sinza, na baadaye viwanja vya leaders club kwa ajili ya kuagwa.
Kwa mujibu wa mwanahabari Zamaradi Mketema ni kuwa miili hiyo ya marehemu (Recho na mwanaye itaagwa na ndugu wa karibu kwa dakika chache nyumbani kwao Sinza na kwenda viwanja vya leaders.
Tukio hilo limeleta simanzi kwa ndugu jamaa na marafiki na vilio ndiyo vimetawala kwa wasanii wa bongo muvi waliofika hospitali ya Muhimbili na kuchukua marehemu.
Social Plugin