TAZAMA PICHA KILICHOJIRI LEO MJINI SHINYANGA,WATUNDE WAZINDUA RASMI KIKUNDI CHAO,NAIBU MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA AONGOZA ZOEZI ZIMA
Saturday, May 31, 2014
Ni katika viwanja vya Mazingira senta mjini Shinyanga ambapo leo kumefanyika uzinduzi rasmi wa kikundi cha WANAWAKE TUNAWEZA NDEMBEZI(WATUNDE) kinachojihusika na shughuli za maendeleo kama vile kuwalipia ada wanafunzi walio katika mazingira magumu na hatarishi zaidi,kutoa huduma ya lishe na vifaa vya usafi kwa wagonjwa walioko majumbani.Pichani wa pili kutoka kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo ndugu David Nkulila ambaye ni naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kikundi hicho chenye makao yake makuu katika kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga.
Katika viwanja vya Mazingira Senta mjini Shinyanga ambako wanawake kutoka manispaa ya Shinyanga walikuwepo kushuhudia uzinduzi wa WATUNDE,kikundi ambapo kilianzishwa tarehe 26.09.2008.Hapa wanawake wanacheza wimbo maarufu kwa jina la Wanawake na Maendeleo.Wa kwanza kushoto ni mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya Shinyanga Pili Misungwi
Mshereheshaji(MC) bi Veronica Isack akifanya yake katika viwanja vya Mazingira senta mjini Shinyanga
Wanawake wakicheza wakati wa uzinduzi wa kikundi cha wanawake Tunaweza Ndembezi.Pamoja na kikundi hicho kuwa na umuhimu mkubwa bado kinakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile upungufu wa fedha katika mfuko wa kikundi jambo ambalo limekuwa likitishia ustawi wa kikundi hicho katika kuwafikia wahitaji zaidi ndani ya manispaa ya Shinyanga.
Aliyesimama ni kaimu afisa maendeleo wa manispaa ya Shinyanga bi Salome Komba akizungumza wakati wa uzinduzi wa WATUNDE ambapo alieleza kuwa kikundi hicho kinafaa kuigwa kwani kimekuwa mstari wa mbele katika kupigania maendeleo ya jamii,mfano hadi sasa kimefanikiwa kusomesha wanafunzi 10 wa shule za sekondari wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi lakini kusaidia wagonjwa majumbani
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika viwanja vya Mazingira senta mjini Shinyanga
Kushoto ni mhasibu wa WATUNDE bi Felister Msemelwa akisoma risala ya kikundi hicho ambapo alisema kikundi hicho kinachoundwa na wanawake kutoka kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga kilianza na wanachama 20 mwaka 2008 mpaka sasa kina wanachama 25 hai wanaosaidiana katika shida na raha wakiwa na dhamira ya kujiwekea akiba katika kikundi ambapo wana akaunti benki ya NMB,wamesajiliwa na wanaongozwa na katiba.Kulia kwake ni katibu wa WATUNDE bi Athanasia Lwamulima
Mgeni rasmi naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila ambaye pia ni diwani wa kata kinakotokea kikundi hicho cha wanawake akizungumza katika uzinduzi wa WATUNDE ambapo aliwataka kuwa na umoja,mshikamano,kupendana na kuepuka kuingiza siasa katika kikundi chao hali ambayo itakifanya kidumu na kuendelea kuwa msaada mkubwa kwa jamii.
Katika kukipongeza kikundi hicho aliwataka wanakikundi hicho kuungana na wadau mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga kupiga vita unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto akitolea mfano wa mtoto Rose Dotto aliyeuawa kikatili mwaka jana ambapo mwili wake uliokotwa ukiwa umewekwa kwenye boksi.
Hata hivyo Nkulila aliiomba ofisi ya ustawi wa jamii katika manispaa ya Shinyanga kuendelea kuhamasisha wadau zikiwemo taasisi kuungana kwa pamoja kufanya maandamano ya amani tarehe 16 Juni 2014 kwenda kwenye kaburi la mtoto Rose Dotto ambalo limejengwa na manispaa ya Shinyanga kama kumbukumbu ya tukio hilo kinyama .
Nkulila alisema kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Anna rose Nyamubi katika kupiga vita ukatili dhidi ya watoto alipendekeza mkuu huyo wa wilaya awe mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika manispaa ya Shinyanga mwaka huu.
Katika uzinduzi huo kulifanyika harambee kuchangia mfuko wa kikundi ambapo shilingi milioni 1 na elfu 24 ambapo katika kukipa nguvu kikundi hicho Nkulila alichangia shilingi laki 2,mbunge wa viti maalum wa CCM mkoa wa Shinyanga Azza Hilal aliyewakilishwa na diwani wa viti maalum CCM wilaya ya Shinyanga mjini Sheila Mshandete amechangia shilingi laki 2 na elfu 50,mbunge wa viti maalum Chadema mkoa wa Shinyanga Rachel Mashishanga aliyewakilishwa na diwani wa kata ya Ibadakuli Leonard James akichangia shilingi shilingi laki 2 na elfu 50
Wageni mbalimbali ,wakiwemo,watoto, wanafunzi wanaosomeshwa na WATUNDE na wagonjwa wa majumbani wakiwa eneo la tukio wakifuatilia kilichokuwa kinajiri
Wa kwanza kulia ni sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Suleiman Kategile akishikana mkono na mmoja wa akina mama wanaosaidiwa na kikundi cha WATUNDE wakati wa zoezi la kukabidhi misaada mbalimbali kama vile sukari,sabuni,mafuta na sembe kwa wagonjwa,watoto na wanafunzi vilivyotolewa na kikundi hicho na kukabidhiwa kwa walengwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila
Katika kufikia malengo waliyojiwekea WATUNDE waliomba kuungwa mkono na wadau mbalimbali ndani na nje ya manispaa ya Shinyanga,msaada ambao utawawezesha kupambana na changamoto kubwa ya ukosefu wa fedha na vitendea kazi pamoja na ofisi rasmi ya WATUNDE.Kama mdau wa maendeleo Unaweza kuwasiliana na mwenyekiti wa WATUNDE bi Agness Makanga kwa simu namba 0769 86 54 77
Mgeni rasmi naibu meya wa Manipaa ya Shinyanga ndugu David Nkulila akikata keki katika eneo la uzinduzi ambapo waliohudhuria wote walipata fursa ya kuila
Mgeni rasmi naibu meya wa Manipaa ya Shinyanga ndugu David Nkulila akimlisha keki mwenyekiti wa WATUNDEbi Agness Makanga
Wageni waalikwa wakiwa katika eneo la uzinduzi ambapo wakati wa harambee ya kuchangia mfuko wa kikundi cha wanawake tunaweza Ndembezi zaidi ya shilingi milioni moja zilipatikana
Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin